Nafasi Ya Matangazo

October 15, 2012

Mabalozi wa Tanga Beach Resort 2012, Happiness Rweyemamu (kulia) na Fina Revocatusi, wakipiga picha ya pamoja wakati wa kukabidhiwa vyeti na zawadi zao za kuwa mabalozi wa TRanga Beach Resort 2012. Warembo hao ni miongoni mwa washiriki wa  Redds Miss Tanzania 2012.
******
Na  Father Kidevu Blog, Tanga
Warembo wawili wanao wania taji la Redds Miss Tanzania 2012, Happiness Rweyemamu (juu) na Fina Revocatusi, (chini) usiku wa kuammkia leo wamechaguliwa kuwa Mabalozi wa Tanga Beach Resort.

Mabalozi hao walipatakina jana katika shindano dogo la kumsaka Balozi wa Hoteli hiyo ya Kitalii ya jijini Tanga kwa warembo hao kupita mbele ya majaji.

Happiness kutoka Kahama Shinyanga na akiwakilisha Kanda ya Ziwa ndie alishika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Fina ambaye anatoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha na anawakilisha Kanda ya Elimu ya Juujijini Dar es Salaam.

  
Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndio waandaji wa Miss Tanzania, Hasim Lundenga amesema mbali ya zawadi y ash laki nne kwa mshindi wa kwanza na Laki mbili kwa mshindi wa pili lakini pia warembo hao wamepata ajira Hotelini hapo.

Warembo walio ingia tano bora ni pamoja na Brigitte Alfred wa Sinza, Happiness Rweyemamu, Fina Revocatus, Diana Hussein na Balozi wa Naura Spring Hotel, Eugene Fabian.


Warembo hao wanao wania taji la Redds Miss Tanzania 2012 wamemalizia ziara yao ya kutembeklea vivutia vya utalii Kanda ya Kaskazini jana katika mkoa wa Tanga kwa kutembelea Mapango ya Kale ya Amboni.
 Mabalozi wa Tanga Beach Resort 2012, wakipiga picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Hoteli hiyo baada ya kukabidhiwa vyeti vyao.
 Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2012 wakipiga picha ya pamoja na Mabalizi wa Tanga Beach Resort.
 Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Tanga Beach Resort, Hamisi Kindoroko (kulia) akimkabidhi zawadi Balozi wa Hoteli hiyo, Hapiness Rweyemamu. Katikati anae shuhudia ni Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga. Mbali na zawadi hizo pia warembo hao walipata mkataba wa ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Tanga Beach Resort, Hamisi Kindoroko (kulia) akimkabidhi cheti Balozi Mdogo wa Hoteli hiyo, Fina Revocatus. Katikati anae shuhudia ni Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga. Mbali na zawadi hizo pia warembo hao walipata mkataba wa ajira.
Posted by MROKI On Monday, October 15, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo