Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited, Bw. Freddie Manento
akibadirishana mkataba na Mkurungenzi wa Kajunason Blog, Bw. Cathbert
Angelo Kajuna mara baada ya Kajunason Blog kuingia mkataba na Push
Mobile kuwawezesha wasomaji mtandao huu kupata habari kupitia simu zao
za mkononi.
Ambapo
mkurugenzi wa kampuni ya Push Mobile alisema kuwa wanafurahishwa na
Kajunason Blog kuingia katika mfumo wa kuwapa habari wasomaji wake kwa
njia ya Simu za Mkononi, “Kajunason Blog ni mtandao wa kwanza kuingia
katika mfumo huu wa kurusha habari kupitia simu za mkononi,” alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kajunason Blog alitoa shukrani zake kwa
kampuni hiyo na kuihakikishia kufanya kazi nao bega kwa bega ili kuweza
kufikia malengo. Pia aliwaomba wasomaji kumuunga mkono kwa kujisajili
ili wafaidike na huduma hiyo kwa kutuma neno KB kwenda 15678.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited, Bw. Freddie Manento
akisaini mkataba wa makubaliano huku pembeni Mkurungenzi wa Kajunason
Blog, Bw. Cathbert Angelo Kajuna akishuhudia. Mkataba huo umesaini ofisi
za Push Mobile jiji Dar es Salaam.
Mkurungenzi
wa Kajunason Blog, Bw. Cathbert Angelo Kajuna akisaini mkataba wa
makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited,
Freddie Manento ambapo Kajunason Blog kuingia mkataba na Push Mobile
kuwawezesha wasomaji mtandao huu kupata habari kutipia simu zao za
mkononi.
0 comments:
Post a Comment