Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete amemteua Prof. Mwajabu Possi kutoka chuo
kikuu cha Dar es salaam kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 8 Octoba, 2012.
Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewateua wajumbe
mbalimbali wa bodi hiyo ambao ni Dkt Mariam Nchimbi, Gideoni Mbalase, Prof.
Elizabeth Kiondo na Balozi Kassim Mwawando.
Wajumbe wengine ni Mkurugenzi
wa Idara ya Habari -MAELEZO Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu
Salva Rweyemamu, Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Zanzibar Omary Chunda pamoja
na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Clement Mshana.
Wakati huo huo Waziri Mkangara
amemteua Christopher Gachuma kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo
Malya.
Aidha amewateua Pendo
Malebeja, William Erio, Richard Ndassa, Lina Kessi, Leornard Thadeo na Allen
Alex kuwa wajumbe wa bodi hiyo.
0 comments:
Post a Comment