Nafasi Ya Matangazo

October 14, 2012

Mrembo wa Ilala, Magdalena Roy, usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kuwa mrembo wa pili kuingia nusu fainali ya Redds Miss Tanzania 2012 baada ya kuwashinda warembo wengine 29 na kutwaa taji la Top Model.

Magdalena aliibuka mshindi katika shindanop dogo la Redds Miss Tanzania lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kimataifa ya Naura Spring jijini Arusha.

Kwa matokeo hayo Top Model, Magadalena Roy anaungana na Miss Photogenic, Lucy Stephano katika nusufainali hiyo na kukaa tayari kusubiri warembo wengine 13 watakaoungana katika Nusu fainali hizo.

Hotel ya Naura Spring pia ilimtangaza Mshiriki kutoka Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa, Egene Fabian kuwa Naura Spring Top Model 2012. 

Taji la TOP MODEL lilikuwa linashikiliwa na mrembo wa Temeke, Mwajabu Juma.
Posted by MROKI On Sunday, October 14, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo