Nafasi Ya Matangazo

October 14, 2012

Mrembo wa Ilala, Magdalena Roy (pichani katikati), usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kunyakua taji la mrembo wa pili kuingia hatua ya nusu fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012 baada ya kuwashinda warembo wengine 29 na kutwaa taji la Top Model.

Magdalena aliibuka mshindi katika shindano dogo la Redd's Miss Tanzania lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kimataifa ya Naura Springs jijini Arusha.

Kwa matokeo hayo Top Model, Magadalena Roy anaungana na Miss Photogenic, Lucy Stephano katika nusu fainali hiyo na kukaa tayari kusubiri warembo wengine 13 watakaoungana katika Nusu fainali hizo.

Taji la TOP MODEL lilikuwa linashikiliwa na mrembo wa Temeke, Mwajabu Juma.








 
Warembo mbalilmabli wa Redds Miss Tanzania wakipita jukwaani wakati wa shindano la Top Model 2012 lililofanyika katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.
Top Model akipita jukwaani 







Mrembo kutoka Mkoa wa Mara na Miss Kanda ya Ziwa 2012, Eugene Fabian nae alifanikiwa kutwaa taji la Ubalozi wa Hotel ya Naura Spring ya jijini Arusha. 

Egene alitangazwa kunyakua taji hilo usiku wa kuamkia leo wakati wa shindano dogo la Redds Miss Tanzania 2012 la kumsaka Top Model ambaye pia ataingia katika hatua ya 15 bora ya Shindano hilo la taifa la Miss Tanzania. Awali taji la Balozi wa Naura Spring Hotel lilikuwa likishikiliwa na Neema Joel.





Posted by MROKI On Sunday, October 14, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo