Warembo
walioingi kwenye hatua ya tano Bora ya Redd's Miss Photo Genic.toka
kulia ni Magdalena Roy (Mshiriki namba 6,kutoka Dar City Center - Kanda
ya Ilala),Babylove Kalala (Mshiriki namba 9,kutoka Kagera - Kanda ya
Ziwa),Lightness Michael (Mshiriki namba 5,kutoka Dodoma - Kanda ya
Kati),Lucy Stephano (Mshiriki namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya
Kaskazini) na Diana Hussein (Mshiriki namba 20,kutoka Dar Indian Ocean -
Kanda ya Kinondoni.)
Mshiriki
namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy Stephano ndie alieweza
kuibuka kinara wa Kinyang'anyiro cha Redd's Miss Photo Genic 2012.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Rino Agency na Muandaani Mkuu wa Mashindano ya Miss
Tanzanzia,Hashim Lundega akitangaza Mshindi wa Redd's Miss Photo Genic
ambaye ni Mshiriki kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy Stephano
(katikati).hafla ya shindano hilo ilifanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa
hoteli ya E'Manyata Lodge,Monduli jijini Arusha.
Warembo
walioingi kwenye hatua ya tano Bora ya Redd's Miss Photo Genic
wakimshangilia mwenzao alieibuka mshindi wa Taji hilo mara baada ya
kutangazwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino Agency na Muandaani Mkuu wa Mashindano ya Miss Tanzanzia,Hashim Lundega.
Warembo wenye vipaji vya kuimba wakitoa Burudani Mbele ya Warembo wenzao wa Redd's Miss Tanzania 2012.
Jaji Mkuu wa Shindano
la Redd's Miss Photogenic 2012,Mroki Mroki asema maneno machache kabla
ya kuanza kutangaza tano bora ya Warembo walioingia kwenye
kinyang'anyiro hicho.
Mkuu wa Itifaki na Nidhamu ya Miss Tanzania,Albert Makoye akitoa muongozo kwa warembo hao.
Na Father Kidevu Blog, Monduli
Mrembo wa Mkoa wa
Manyara, na mwakilishi wa Kanda ya Kaskazini, Lucy Stephano usiku wa kuamkia
leo amenyakua taji la Redds Miss Photogenic 2012 na kuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali
ya shindano la Redds Miss Tanzania 2012.
Lucy amefanikiwa
kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo
wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2012.
Shindano hilo dogo la
Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana
baada ya jopo la majaji ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania
wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki.
Mapema akitaja majina
ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine
aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha Othman Michuzi na Katibu Mkuu wa Kamati
ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.
Dalili za kuonesha kuwa
Lucy amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka
wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na
lilipotajwa jina lake ukumbi wa Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na
warembo ulilipuka kwa kwashangwe.
Warembo watano
walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Magdalena Roy, Lightness Michael,
Babylove Kalala, Diana Hussein na Lucy Stephano.
Warembo wa Redds Miss
Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji
kufanyika Oktoba 13 2012, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.
Mataji mengine yatakayo
waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu
fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.
Taji la Miss Photogenic
lilikuwa linashikiliwa na mrembo Stacy Mabula kutoka Shinyanga na Kanda ya
Ziwa.
Fainali za mwaka huu za
Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Blue Peal Ubungo
jijini Dar es Salaam Novemba 2, 2012.
0 comments:
Post a Comment