Mkuu wa
Wilaya ya Magu, Mh Jaqueline Liana akikata utepe wakati wa uzinduzi wa
uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa katika Kijiji cha Bugabu
uliofadhiriwa na kampuni ya Alpha Choice ya Mwanza.
Mkuu wa
Wilaya ya Magu, Mh Jaqueline Liana akifungua bomba la maji kuashiria
uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa katika Kijiji cha Bugabu
uliofadhiriwa na kampuni ya Alpha Choice ya Mwanza.
Mkuu wa
Wilaya ya Magu, Mh Jaqueline Liana akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa
kijiji cha Bugabu,wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa katika
Kijiji cha Bugabu uliofadhiriwa na kampuni ya Alpha Choice ya Mwanza.
******
Mkuu wa
Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana amempa saa 24 Mkuu wa Idara ya Maji wa
wilaya hiyo kuwasilisha ripoti ya mradi wa maji uliojengwa katika Kijiji
cha Bugabu uliofadhiliwa na kampuni ya Alpha Choice ya Mwanza.
Amri hiyo ya Liana inatokana na malalamiko ya wananchi wa kijiji cha
Bugabu wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa maji uliogharimu kiasi cha
zaidi ya shilingi million 5.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo wa maji utakaosaidia wananchi wa
vijiji vitatu, Jaqueline Liana amesema kumekuwa na tabia kwa wakuu wa
idara na viongozi wa vijiji kutosoma mapato na matumizi ya miradi.
Amesema
kuwepo kwa usiri katika miradi mbalimbali kunawafanya wananchi kuichukua
serikali yao,kitu ambacho kinaweza kuepukwa iwapo suala la kusomwa
mapato na matumizi litazingatiwa. Afisa mtendaji wa kijiji cha Bugabu
Rebecca Jonas na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamezungumzia
changamoto mbalimbali kuhusiana na mradi huo wa maji
Meneja
mauzo wa Kampuni ya Alpha Choice inayomiliki viwanda vya kusindika
minofu ya samaki katika nchi za Afrika Mashariki Bruno Mhoja amesema
mradi huo wa maji ni makakati wa kampuni kushirikiana na jamii katika
miradi ya maendeleo.
Mradi huo wa maji ni wa kwanza katika kijiji cha Bugabu kutolewa na wawekezaji ambao utawanufaisha wananchi zaidi ya laki moja.
0 comments:
Post a Comment