Mfanyabiashara
maarufu mkoani Iringa na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Salim Abri
Asas ( wa pili kulia) akikabidhi msaada wa mifuko 200 ya saruji yenye
thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 3 .2 kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw
Gerald Guninita hivi karibuni ofisini kwake, wanaoshuhudia ni
mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Joseph Mhumba ,kushoto na
mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo Momahend Gwalima.
wadau wa elimu wilaya ya Kilolo wakiwa na mfanyabiashara Salim Asas
KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Salim Abri Asas ametoa msaada wa mifuko 200 ya Saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.2 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule nne za sekondari wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Akikabidhi msaada huo ofisini kwake, Asas alisema kuwa amelazimika kuchangia ujenzi huo wa mabweni ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Jakaya Kikwete ambapo suala la elimu limekuwa likipewa kipaumbele zaidi.
Alisema kuwa mbali ya kuchangia ujenzi huo katika wilaya ya Kilolo pia amepata kufanya hivyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na maeneo mengine ya mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa wilaya hiyo ya Kilolo kupitia mkuu wa wilaya Gerald Guninita waliandika barua kwake kuomba kusaidiwa ujenzi wa shule za sekondari na mabweni katika wilaya hiyo ya Kilolo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Guninita mbali ya kumpongeza Asas ambaye pia ni mmoja kati ya wafanyabiashara mkoani Iringa bado aliomba wadau wengine wa elimu katika mkoa wa Iringa wakiwemo wafanyabiashara kujitokeza kuchangia maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo ya Kilolo.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa saruji hiyo itagawanywa mifuko 50 kwa shule nne za sekondari ambazo zinaendelea na ujenzi wa mabweni ya watoto wa kike.
Alizitaja shule za sekondari ambazo zitanufaika na msaada huo kuwa ni sekondari ya Uhambingeto,Gangwa ,Ukwega na Masisiwe .
Aidha mkuu huyo wa wilaya ametangaza kuwachukulia hatua kali wale wote wanaowapa mimba wanafunzi na kuwa tayari ameagiza viongozi kuanza kuwasaka wahusika wa mimba za wanafunzi ili kukamatwa na kufikishwa mahakamani.Habari picha kwa hisani ya mdau Francis Godwin-Iringa.
0 comments:
Post a Comment