Rais wa UTPC Keneth Simbaya (kushoto) na Katibu Msaidizi IPC, Frncis Godwin wakiongoza waombolezaji walio fika Tukuyu, kubeba jeneza jana wakati ya mazishi ya Shujaa Daudi Mwangozi aliyekuwa Mwakilishi wa Kituo cha televisheni cha Channel Ten mkoani Iringa aliyeuwawa kikatili wakati akishambuliwa na Polisi katika Vurugu za Chadema na Jeshi hilo akiwa anatekeleza majukumu yake ya kila siku ya utafutaji Habari. Shujaa Daudi Mwangosi alizikwa kijijini kwao Tukuyu Septemba 4, 2012.
Mjane wa Marehemu, Shujaa Daudi Mwangosi akilia kwa uchungu mkubwa huku akiwa amelala juu ya Kabuuri la Mpedwa Mumewake. Machozi ya mjane huyu na watoto, Ndugu jamaa na marafiki wote wa Marehemu pamoja na Damu isiyo na hatia ya Daud Mwangosi katu havitaweza kupotea bure na Mungu atajibu kwa wale wote walio msababishia mama huyu na watoto wake wan ne kubaki wakiwa.
Umati wawatu uliofurika kumzika Shujaa Daudi Mwangosi.
Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akilia kwa uchungu wakati akitoa heshima za mwisho kwa mpedwa mumewe.
Watoto wa marehemu wakiweka mashada ya maua juu ya kaburi la baba yako Kiopenzi Shujaa Daudi Mwangosi
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Mark Mwandosya akiweka Shada la maua katika kaburi la Shujaa Daudi Mwangosi. Hii ndio safari ya mnwisho ya mpendwa wetu Daud Mwangosi, Shujaa wa taaluma ya Habari aliyeuwawa wakati akitekeleza majukumu yake ya Uandishi wa habari mkoani Iringa.
0 comments:
Post a Comment