Nafasi Ya Matangazo

September 04, 2012



 Kushoto Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais bw. Richad Muyungi kulia ni Rais wa mkutano wa dunia wa 18 wa mabadiliko ya tabianchi ambae pia ni Naibu waziri mkuu wa Qatar mh. bw.Abdullah Bin Hamad Al Attiyah mara tuu baada ya mkutano wa kusikia mategemeo wa washiriki wa mkutano wa Disemba, katika mkutano wa kimataifa unaendelea mjini Bangkok.


Mkurugenzi msaidizi idara ya mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Richard Muyungi, (kushoto) akitoa maelekezo kwa afisa mazingira mwandamizi kutoka ofisi ya makamu wa rais mazingira bi Emelda Teikwa katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi unaondelea mjini Bangkok.

***************
Rais wa mkutano wa 18 wa Dunia wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika mjini Doha mwishoni mwa mwaka huu, amekutana na wenyeviti wa bodi mbalimbali za mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Bangkok, akiwa na lengo la kujitambulisha na kusikia mategemeo ya washiriki katika mkutano ujao.

Baadhi ya washiriki waliopata nafasi ya kutoa mategemeo yao leo, ni pamoja na mwenyekiti wa kundi la Africa kutoka nchini Swazland, akizungumza kwa niaba ya Afrika alisema kuwa, Anaamini kuwa mazungumzo yote ya majadiliano yanayoendelea hapa Bangkok yatakuwa na mafanikio katika mkutano wa Doha kwani yoote yapo ndani ya uwezo wa washiriki wote, na kundi la nchi zilizoendelea wanatakiwa kutimiza  “commitiment” zao ili kuweza kufikia malengo.

Aliongeza kwa kusema kuwa, anaamini kila upande una jukumu la kuufanya mkutano wa Doha kuwa na mafanikio kwani “wote tunajua na tumeona madhara makubwa na  athari zitokanazo na  mabadiliko ya tabia nchi hivyo basi sote tuna wajibu wa kukabiliana na athari hizo. Alisisitiza”

Aidha, mwakilishi huyo wa Afrika alisema kuwa ni vizuri kikaangaliwa kile kinachotakiwa kufanyika mpaka kufikia mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na hatua za kuchukua, na kufikia malengo  ya kupunguza joto la dunia.

Kwa upande wake Rais wa mkutano  wa  18 wa Dunia wa  mabadiliko ya tabianchi ambaye pia ni Naimu waziri mkuu w anchi ya Qatar,  amewakaribisha washiriki wote na kusema kuwa yupo tayari kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kufikia malengo katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Posted by MROKI On Tuesday, September 04, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo