Habari za hivi punde; Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Daudi Mwangosi, pichani - amefariki dunia kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa baada ya kutokea vurugu baina ya polisi na wafuasi wa chama cha Chadema.
Habari zilizotufikia kutoka huko, zinadai kuwa Mwangosi, ambaye ni mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Channel ten, amefariki papo hapo.
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo
Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii nchi kwakweli sijui tunaenda wapi? Hii ndio serikali police wametumwa na serikali, kwani wangewaacha hao chadema yte yangetokea kweli, mi naomba hao mapolice tuliowaona kwenye vyombo vya habari akimzunguka marehemu nao wauliwe. Na waaandishi wa habari wasitoe taharifa yoyote ile ya police wala viongozi waserikalini, maana ndio haohao wanaochochea mauaji, juzi tu ilikuwa morogoro leo imekuwa iringa kesho tena itakuwa na mkoa mwingine,
ReplyDelete