Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Street Children Sports Academy TSC ya Mwanza Bw. Mutani Yangwe akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Karume wakati akielezea mafanikio ya timu ya Academy yao waliyoyapata kutoka nchini Ujerumani na kunyakua mataji mbalimbali na zawadi kemkem. amesema takribani wachezaji saba wamefanikiwa kupata ofa ya kufanya majairibio nje watatu wakihitajika katika timu ya Makabi Haifa ya Israel na wengine wanne wakipata ofa kwenda nchini Sweden ambako watapitia kisha kwenda nchini Ujerumani. Katikati katika picha ni Altaf Hirani Rais wa kituo hicho na kushoto ni kocha wa kutuo hicho Bw. Rogashian Kaijage
Altaf Hirani Rais wa Taasisi ya Tanzania Street Children Sports Academy TSC ya Mwanza akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF kulia ni Mkurugenzi wa TCS Mutani Yangwe na kushoto ni Mmoja wa maofisa wa kituo hicho B. Leonard Magomba.
Viongozi wa kituo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo kutoka TCS Mwanza mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakiwa na mataji yao waliyoijishindia na zawadi mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment