Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu
Someni kituko hiki anachosimulia DC wa Handeni, Muhingo Rweyemamu juu ya mzee mmoja aliyeoza binti zake wakiwa shule.
"Niwape kituko cha Handeni. Tumemkamata mzee mmoja aliyekubali kupokea mahari ya binti yake akiwa kidato cha tatu kwa makubaliano tu kwamba akimaliza kidato cha nne, basi achukuliwe juu kwa juu. Binti ana umri wa miaka 17.
Hata hivyo, binti akiwa bado kidato cha tatu, akapata mimba ya kijana mwingine. Huyo kijana ni wa kijiji cha Kang'ata wakati mzee na mabinti zake ni wa kijiji cha Kwachaga.
Sasa huyu aliyeleta mahari alipopata habari, akarudi kijijini ili kuthibitisha habari hizo. Walifanya mazungumzo na jamaa akakataa kurudiwshiwa mahari yake. Akataka apewe binti wa darasa la sita badala ya huyu mkubwa wa kidato cha tatu.
Mzee mwenye mabinti hakuwa na jinsi isipokuwa kumtoa huyu binti mdogo wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 15. Waliondoka na huyo binti kwenda Dar es Salaam. Nilipopata habari na kuanza uchunguzi, mzee akashtuka akaagiza bibi harusi arudishwe haraka.
Kumbe tulikwishaweka mitego shuleni. Alimrudisha ili aje kuzuga shuleni na wasubiri shule zifungwe ili waondoke kwa amani.
Siku moja kabla ya shule kufungwa nikalituma jeshi la polisi kijijini hapo nikasomba baba, mama na mabinti wote wawili na kuwapeleka hospitali kisha polisi.
Binti mkubwa mimba ya miezi saba lakini mdogo bado hajapata mimba ila ameharibiwa. Baba na binti mkubwa nikawaweka kwanza kituoni ili tupata mtia mimba na muoaji kwanza". Habari ndiyo hiyo
0 comments:
Post a Comment