Nafasi Ya Matangazo

August 27, 2012

Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi akionyeshwa sehemu ya madarasa ya shule ya msingi Singisa ambayo kuta zake zilianguka miaka miwili iliyopita na mpaka leo hazijakarabatiwa kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara.
Operesheni Sangara zinazoendelea Morogoro bado zimeendelea kuwa chachu ya kuimarisha CHADEMA katika kila vijiji wanavyofikia. Picha hizi ni katika kijiji ambacho hakuna zahanati na kina shule moja tu ya Msingi yenye wanafunzi 398 na Mwalimu mmoja tu!!Wanafunzi wote wanakaa chini. Kijiji hiki ifahamike ndicho pia makao makuu ya tarafa na kata ya Singisa.(Kata ya Singisa ina vijiji 7). Makao Makuu ya Kata ndipo pia mwisho wa barabara, hivyo vijiji vingine sita havifikiki na vimetengwa kabisa kimawasiliano.

Moja ya lalamiko kubwa la wananchi, wamekuwa wakichangishwa michango isiyo na idadi na serikali ya kijii huku wakiwa hawasomewi mapato na matumizi. Baada ya elimu hasa ya uraia na umuhimu wa haki yao hiyo iliyotolewa na CHADEMA, wanakijiji wameapa ndani ya wiki mbili wataitisha mkutano wa kijiji na kuwatimua madarakani viongozi wa kijiji baada ya kuenda kinyume na taratibu za kuendesha serikali ya kijiji.

Hapa CHADEMA kupitia Katibu Mkuu, BAVICHA Bw. Deogratias Munishi wamezindua Tawi lenye wanachama 52 na wananchi wamepata fursa kuunda uongozi wao wa CHADEMA.
Posted by MROKI On Monday, August 27, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo