NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Dkt. Julius Rotich (pichani) anataraji kufungua mafunzo ya siku tatu ya upigaji picha yajulikanayo kama ‘EAC-GIZ Master Class Photographers Training’ yatakayo anza Julai 23-26, 2012 mjini Arusha.
Juma la wapigapicha 10 kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki wanataraji kuhudhuria mafunzo hayo ya siku tatu ya Upigaji yatakayofanyika katika Hotel mjini Arusha.
Mafunzo hayo ya nadharia na vitendo yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jumuia ya Afrika Mashariki na Shirika la Kijerumani (EAC) na GIZ yatahusiha wapigapicha hao kumi, wawili kutoka kila nchi.
Tanzania inawakilishwa na Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti na Habari za Mtandao, Mroki Mroki, Mwasisi na Mhariri Mkuu wa FATHER KIDEVU BLOG pamoja na Mwandshi wa Kampuni ya Mwanachi Comunication mjini Arusha, Filbert Rweyemamu.
Tayari wapigapicha hao wa Habari wapo mkoani Arusha wakiwasubiri wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuwasili kwa kuanza mafunzo hayo.
Mkufunzi wa mafunzo hayo ni Balozi wa Heshima wa Utalii nchini Kenya na Mwenyekiti wa mfuko wa 50 Treasures of Kenya, Hartmut Fiebig.
0 comments:
Post a Comment