Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuo Hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa Wanasubiri Kwenda Kutoa damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akiaga wanafunzi na wafanyakazi waliojitoa katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) lililofanyika chuo hapo leo.
Picha Zaidi bofya http://josephatlukaza. blogspot.com
0 comments:
Post a Comment