Nafasi Ya Matangazo

June 13, 2012

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya taifa ya mchezo wa Pool kwa mwaka huu. Mashindano haya yajulikanayo kama “Safari Lager National Pool Championships 2012” yanafanyika kwa mwaka wa tano sasa, Safari Lager imekuwa wadhamini wakuu wa mashindano haya kwa miaka yotemitano.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Meneja wa Bia ya  Safari Lager Bwana Oscar Shelukindo alisema;“Nia hasa ya kudhamini mashindano haya ni kuibua vipaji kwa vijana na kuwasaidia kiuchumi hasa ukizingatia kwamba kwa sasa michezo ni ajira kama ajira nyinginezo.

Mchezo wa pool huandamana pia naburudani waipatayo wachezaji kutokana na mchezo huo”. Bw. Shelukindo aliendelea kusema; “Ukiachilia mbali ongezeko la kipato na burudani, mchezo wa pool husaidia kuwakutanisha watu mbalimbali kufahamiana kibinafsi na kibiashara, hujenga afya bora na katika mazingira yetu ya sasa michezo inamsaidia mtu kutumia muda wake vizuri ili kuepuka mambo mengine yanayoweza kumsababishia matatizo kama vile kukaa vijiweni, ugomvi nk”.

Mashindano yaliyomalizika ya mchezo wa Pool kwa vyuo vikuu mwaka huu yalikuwa na ujumbe; Play Pool, Stay Cool.. hii ikiwa na maana ya kuwashauri wanavyuo kucheza Pool na kubakia watulivu... wasio na matata!.. Mashindano ya kitaifa ya pool kwa vyuo vikuu yalifanyika mkoani Iringa ambapo chuo cha SAUT cha mkoani Mwanza kiliibuka kidedea baada ya kuwachapa chuo cha IFM cha Dar Es Salaam!.

Safari Lager imekuwa wadhamini wa mchezo wa Pool toka mwaka 2008, imedhamini mashindano ya ndani na ya nje ya nchi pia. Imedhamini timu ya Taifa ya mchezo wa Pool kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa Pool nchini Ufaransa mwezi wa kumi mwaka 2010 ambapo timu yetu ilifanya vizuri. Mashindano ya kimataifa ya mchezo wa Pool yatafanyika katikati ya mwezi wa kumi nchini Uingereza, katika mji wa Blackpool.

Naye Bw. Amos Kafwinga, katibu wa chama cha mchezo wa Pool Tanzania (TAPA) alisema mashindano ya mwaka huu yana mvuto wa aina yake kwani katika ngazi ya taifa yatahusisha vilabu na sio mikoa kama miaka ya nyuma. “Mashindano yataanzia mikoani kwa Vilabu kushindana katika ngazi ya Mkoa na baadae vilabu vilivyoshinda katika ngazi ya mkoa vitawakilisha mikoa yao na kushindana katika ngazi ya Taifa ili kupata clabu ambayo ni mshindi wa jumla kwa vilabu vya Mikoa yote’.

Mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kuanza rasmi kutimua vumbi katika mkoa wa Tanga Juni 21 mwaka huu. Mashindano haya yatahusisha vilabu katika Mikoa 16, ambayo ni Tanga, Manyara,Kilimanjaro,Arusha,Iringa,Mbeya,Dodoma,Morogoro,Shinyanga,Mwanza,Tabora,Kagera,Lindi,Temeke,Ilala na Kinondoni. Mashindano ya mwaka huu yameongeza mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Tabora na Lindi. Fainali za vilabu kitaifa zitafanyika katika mkoa wa Mwanza mwishoni mwa mwezi Septemba.

Mwaka jana mashindano ya taifa yalihusisha timu za mikoa ambapo Mkoa wa Dodoma waliibuka mabingwa baada ya kuwatoa mkoa wa kimashindano wa Temeke. Mashindano ya mwaka jana yalifanyika mkoani Dodoma. Timu ya Dodoma  walijipatia kikombe,medali za dhahabu na jumla ya shilingi milioni tano taslimu.

Akito ashukran ikwa Safari Lager kwaniabaya Chama cha Mchezowa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chamahicho Bw. Isaac Togocho alisema “Taswira ya mchezowa pool apa nchini imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa inawavutia vijana mbalimbali kwani simchezo wa kupotezea mudatena kama wengi walivyodhania, pool miongoni mwa michezo inayokua kwa kasikubwa na kuwapatiakipatowachezajinavijanakwaujumla.

Hiiyo imetoka na Biaya Safari Lager kukubali kuudhamini mchezo wa Pool table. Kwaniaba ya chama tunatoa shukrani nyingi sana na kuomba Safari Lager iwenasi ilituendelee mbelezaidi”.
Bwana  Oscar alizita ja zawadi za washindi katika ngazi ya mikoa kuwa timu itakayoshindaitajipatiakitita cha shilingilakisaba, washindiwenginewatajipatiashilingilakitatunanusukwamshindiwapili, lakimbilikwamshindiwatatunalakimojakwamshindiwanne. Washindikwaupandewamchezajimmojammojawakiumewatajipatiashilingilakitatunanusukwabingwanalakimbilikwamshindiwapili. Wachezajiwa kike watachuanapiaambapowashindiwatajipatialakimbilinanusukwabingwanashilingilakimojananusukwamshindiwapili.
Timuitakayoibukamshindikatikangaziyataifaitaibukanakikombepamojanamedalizadhahabuzawadihizizitaandamananazawadiyajumlayashilingimilionitanotaslim. Jumlazaidiyashilingimilionihamsininasabazitatolewakamazawadizapesataslimukatikamichuanoyamwakahuu.
Bwana Oscar alimaliziakwakutoashukranikwawanywajiwabiaya Safari Lager nawachezajiwotewamchezowa Pool kwaujumla, aliwaombawachezajiwajinoezaidiilikufurahiazawadizamwakahuu.
Posted by MROKI On Wednesday, June 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo