Nafasi Ya Matangazo

June 04, 2012

 Timu ya Soka ya  Tanzania ‘Taifa Stars’ jana ilikipiga na timu ya Taifa ya Ivory Coast katika mchunuano wa awal;I wa kuwania kufuzi kucheza Kombe la Dunia. Katika Mchezo huo ulipigwa Ivory Coast Timu ya Taifa Stars ilifungwa kwa taabu magoli 2-0 na wakali hao wa soka barani Afrika.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mpya wa timu hiyo Kim Polsen licha ya kufungwa magopli mawili lakini Watanzania walio wengi wameipongeza timu hiyo kwa mchezo mzuri na wa kiwango walio uonesha na kudai kuwa kiwango cha Tanzania na Ivory Coast hakiupaswa kuwa hivyo bali ni zaidi ya goli 5.

Pichani ni Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta akiwania mpira na Alexander Igor Lolo wa Ivory Coast
 Wachezaji wa akiba wakifuatilia kwa makini wakati wa mechi dhidi ya Ivory Coast jana.
 Vikosi vya Taifa Stars na Ivory Coast vikiingia uwanjani kuanza pambano lao jana.
Beki Siaka Tiene (kulia) akimfanyia madhambi Mrisho Ngassa wa Taifa Stars wakati wa mechi hiyo iliyofanyika jana.

 Mbwana Samatta wa Taifa Stars akiwania mpira na Salomon Kalou wa Ivory Coast.
 Gervais Yao 'Gervinho' wa Ivory Coast akimtoka Amir Maftah wa Taifa Stars
Mshambuliaji Mrisho Ngassa (kushoto) wa Taifa Stars akiwania mpira na Kolo Toure wa Ivory Coast.
Posted by MROKI On Monday, June 04, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo