Nafasi Ya Matangazo

June 08, 2012

 Miss Utalii Tanzania 2012- Kandaya Ziwa, wakiwa wamepozi katika hoteli ya Monarch ambako kambi ya Mazoeziinaendelea, tayari kwa Fainali itakayo fanyika hotelini hapo 30-6-2012.
**********
Bodi ya Taifa yaMashindano ya Miss Utalii Tanzania, katika kutekelezaa mpango mkakati wake wakuimarlisha na kuboresha zaidi mashindano hayo, imegawanya mikoa yote ya Tanzaniana Vyuo Vikuu katika kanda maalumu za mashindano hayo.

Kwa lengo lakuimalisha utekelezaji wa malengo ya mashindano na usimamizi , Kuanzia mwakahuu kutakuwa na jumla ya kanda 14 za mashindano ya Miss Utalii Tanzania ,zikiwemo saba (7) za kawaida na saba (7) kanda maalumu za Miss Utalii vyuo Vikuu.Hatua inalenga pia kufikisha mashindano ya Miss Utalii Tanzania hatika Ngazi zachini zaidi , mijini na vijijini, ambapo kwa kuanzia mashindano haya sasayataanzia katika Ngazi za kata, Majimbo ,Wilaya,mikoa, kanda, taifa na hatimayeDunia, hiku mpango mkakati ni kuanza kufanyika katika mgazi za vijiji ifikapomwaka 2014. Huu ni mpango wa lazima kwetu kwa mujibu wa kanuni na taratibu zamashindano haya, ambayo pamoja na malengo mengine yanalenga pia kuelimisha nakuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa sekta ya Utalii kiuchumi na kijamii,hivyokuwa fulsa pekee ya kufanyika kwa mashindano haya katika Ngazi za vijijilufikia mwaka huo 2014.

Mgawanyo wa kanda hizona mikoa yake katika mabano ni:

A: KANDA ZA KAWAIDANI:

1.      Miss Utalii Tanzania –Kanda ya Mashariki  (Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara,Zanzibar)
2.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Magharibi (Simiyu, Shinyanga na Mara)
3.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Ziwa (Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma)
4.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro na Arusha)
5.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kati  (Tabora, Dodoma, Singida na Morogoro)
6.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya  KusiniNyanda za Juu  (Mbeya, Rukwa na Katavi)
7.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kusini  (Ruvuma, Iringa na Njombe)

B: KANDA MAALUM ZAVYUO VIKUU NI:

1.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kati (Dodoma, Kigoma,Tabora, Singida)
2.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kusini (Iringa, Ruvuma, Njombe)
3.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Pwani  (Dar es Salaam, Zanzibar , Lindi na Mtwara)
4.  Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu- Kanda ya Magharibi (Mwanza, Geita, Kagera,Mara, Simiyu, Shinyanga na Singida) 
5.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kusini Nyanda za Juu  (Mbeya, Rukwa, Katavi)
6.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kaskazini ( Arusha,Kilimanjaro,Manyara)
7.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Mashariki (Morogoro, Mtwarana Lindi)

Mgawanyo huu wa kandaumezingatia , maeneo ya kijografia, mwingiliano wa tamaduni, uwepo wa vivutiovya Utalii katika kila kanda, urahisi wa kutangaza Utalii na kuhamasisha Utaliiwa ndani,pia kutoa fulsa kwa mabinti wengi zaidi kushiriki mashindano hayakatika Ngazi zote.

Aidha mfumo huu,utasaidia kuwachuja washiriki katika Ngazi za kanda, hivyo kuwa na washirikiwenye viwango na ushindani unaokibalika kwa mujibu wa kanuni na taratibu zamashindano haya na mengine yahusuyo kitaifa na kimataifa.

 Kwa mwaka huu, kandaya ziwa ndiyo itakayo kuwa ya kwanza kufanya Fainali zake za Miss Utalii Kandaya Ziwa 2012 na kushirikisha jumla ya warembo 15 kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera,Geita na Kigoma. Shindano hilo linalo andaliwa na Fania Hassani ambaye niMkurugenzi wa Miss tourism Tanzania Organisation kanda ya Ziwa na Fania BeautySaloon ya limepangwa kufanyika Juni 30, 2012 katika ukumbi wa Monarch Hotel Mwanzana kudhaminiwa na Gold Masters, Monarch Hotel, Garrett Security Items na SolarPower MSP – H na magazeti ya Gazeti la Jambo Leo, KIU Investment.
Posted by MROKI On Friday, June 08, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo