Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Maarifa Mwl Marietha Mulyalya wakati Airtel ilipotembelea shule za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika Gongolamboto na kukabidhi vifaa vya michezo hapo Jana
Walimu wa shule za msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika wakiwa na jezi zao mara baada ya kukabithi vifaa vya michezo na Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel, makabithiano hayo yalifanyika katika shule ya msingi Maarifa Gongolamboto jijini Dar es Saalam. Pichani (Katikati) ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde
Walimu wa shule za msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika wakiteja jambo mara baada ya kukabithiwa vifaa vya michezo na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Kikundi cha kwaya cha shule ya msingi ya Maarifa kitumbuiza wakati wa hafla ya kukabithiwa vifaa vya michezo illiyofanywa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika shule ya msingi Maarifa Gongolamboto jijini Dar esa saalam.
*****
shule za msingi zilizoko Gongolamboto Dar es saalam zimenufaika na vifaa
vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel jana
katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya msingi maarif. Airtel imetoa
vifaa vya michezo lengo likiwa ni kuleta hamasa na kuwajenga wanafunzi
katika mchezo wa soko wakiwa mashuleni na katika umri mdogo.
Vifaa hivyo vya michezo vimetolewa na Airtel kwa shule za Msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika ambapo kila shule ilipata seti moja
ya jezi na Mipira. Akiongea mara baada ya kupokea vifaa hivyo mkuu wa shule ya maarifa Bi Marieta Mulyalya alisema “ Natoa shukurani zangu za dhati kwa Airtel kwa kutoa vifaa vya michezo kwa shule za Gongolamboto na kuahidi kuvitumia vizuri kwa manufaa ya shule na wanafunzi na washukuru Airtel kwa msaada wa madawati ambayo walituleate wiki chache zilizopita na tunawaomba Airtel waendelee kutoa msaada si kwa shule yake tu bali na kwa shule za jirani pia ambazo pia zina mahitaji Mengi”.
Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Airtel inatambua mchango wa michezo mashuleni na katika kuendeleza kuinua kiwango cha soka nchini ndio maana tunaendelea kuwawezesha wanafunzi hawa kuendeleza mchezo wa mpira kwa kuchangia vifaa hivi muhimu. Tunaamini
jezi hizi zitatumika katika michuano mbalimbali shule ili kuwawezesha
kukuza vipaji vyao ambapo matokeo yake ni kuzalisha kikosi kizuri cha timu
ya taifa”.
Mwenzi uliopita Airtel ilitoa madawati kwa shule ya Maarifa na kuwawezesha
wanafunzi kupata madawati ya kukali ambayo ilikuwa changamoto kubwa shuleni
hapa kwasababu shule hzo ni kati ya shule zilizoathiriwa na mlipuko wa
mabomu uliotokea katika ghala la kuifadhia silaa la Gongolamboto.
“leo tunayofuraha kuwapatia vifaa vya michezo shule ya maarifa pamoja na
shule za jirani za Mwangaza na Gongolamboto Jaika, Airtel bado inaendelea
kutoa vifaa vya michezo ambapo hivi karibuni inategemea kugawa vifaa vya
michezo kwa Zaidi ya shule kumi zilizoko Nyanda za juu kusini ikiwemo mikoa
ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, Songea na Rukwa” alimalizia kusema Bi Matinde.
Airtel imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika sekta ya michezo lengo likiwa ni kukuza maendeleo ya michezo hapa nchini, mwaka huu Airtel kwa
mara nyingine iimeendelea kuendesha program yake ya kuinua vipaji vya vijana chini ya miaka 17 ijulikanayo kama Airtel Rising Stars ambapo vijana
wengi wameweza kufaidika na program hiyo.
0 comments:
Post a Comment