Watanzania
kutoka kila kona ya Roma nchini Italia, wakiongozwa na balozi wa
Tanzania nchini Italia, Mheshimiwa James Msekela, pamoja na marafiki
mbalimbali wa marehemu James A. Mbwana, walikusanyika kwenye misa
takatifu ya kuuaga mwili wa marehemu aliyefariki gafla jumatano tarehe
16 mei 2012 maeneo ya Termini mjini Roma akiwa njiani kuelekea Chuoni
kama ilivyokuwa kawaida yake.
Misa
hii imefanyika katika parokia ya Mtakatifu Francisco jimboni Palestrina
mjini Roma ambako marehemu alikuwa akitumikia na kuishi sambamba na
kufuatilia masomo yake katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino
kilichopo mjini Roma. Misa iliongozwa na Mhasham Askofu Dominic, Askofu
wa Jimbo la Palestrina.
Habari
zaidi juu ya lini mwili wa marehemu utaondoka tutawapatieni kadri
tutakapo zipata. Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania Roma tunawapa pole
sana ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa ambao unatukumbusha
kuwa sisi binadamu hapa duniani ni wapita njia tu. Siku yoyote mwenyezi
Mungu anaweza kutuchukua. Kwa hiyo hatuna budi kujiandaa kwa kusali na
kutenda mema mbele ya mwenyezi Mungu.
Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake liidimiwe milele amina!
Jeneza la Marehemu Fr. James Mbwana likiwa kanisani wakati wa misa.
Kutoka Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. James Msekela pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Leonce Uwandameno wakati wa ibada takatifu.
Ibada ikiendelea.
Kwa habari zaidi tafadhali tembeleeni www.watanzania-roma.blogspot. com
0 comments:
Post a Comment