President
Jakaya Kikwete speaks at the Centre for Strategic and International
Studies (CSIS) during a Stateman's forum on development themed "A
country Transformed: A New Agenda for Tanzania".
President
Barak Obama of the United States of America mingles with the crowd
after delivering his Keynote Speech at the opening of the symposium
themed "Food Security at the G-8: Changing the development landscape" at
the Ronald Reagan building and International Trade Centre in Washington
DC.
President
Jakaya Kikwete meets UK's Secretary of State for International
Cooperation Hon Andrew Mitchel in the sidelines of the symposium themed
"Food Security at the G-8: Changing the development landscape" at the
Ronald Reagan building and International Trade Centre in Washington DC.
US
Secretary of State Hillary Clinton for a souvenir wraps up the
symposium themed "Food Security at the G-8: Changing the development
landscape" at the Ronald Reagan building and International Trade Centre
in Washington DC.
President
Barak Obama of the United States of America introduces President Jakaya
Kikwete as he acknowledges the presence of four African leaders present
symposium themed "Food Security at the G-8: Changing the development
landscape" at the Ronald Reagan building and International Trade Centre
in Washington DC. The session outlined key components of the G8
deliverables for food and nutrition security. Others were HE Meles
Zenawi, Prime Minister of Ethiopia, Prof. John Evans Atta Mills,
President of Ghana and African Union Chairman and President of Benin, HE
Dr Boni Yayi.
Tanzania's
envoy to the US Ambassador Mwanaidi Sinare Maajar with the Permanent
Representative of the African Union to the UN. Ambassador Amina Salum
Ali and Senior advisor to the President of Tanzania (Diplomacy)
Ambassador Liberata Mulamula take a break after a consultation meeting
of leadership on the follow-up of G-8 commitments on the sidelines of
the symposium themed "Food Security at the G-8: Changing the
development landscape" at the Ronald Reagan building and International
Trade Centre in Washington DC.
****
Na Mwandishi Maalum
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete yuko Marekani
kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Tajiri Zaidi na Zenye Viwanda
Duniani (Group of Eight – G-8) kwa mwaliko wa mwenyeji wa Mkutano huo
Rais Barack Hussein Obama wa Marekani.
Rais Obama amewaalika,
kama wageni rasmi, marais wa nchi nne za Afrika kuhudhuria mkutano huo
ambao shughuli zake zilianza juzi – Alhamisi, Mei 17, 2012 kwa wakuu hao
kukutana na kuhuduria tafrija rasmi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani Mama Hillary Rodham Clinton katika Wizara ya Mambo ya Nje ya
Marekani mjini Washington.
Jana, marais hao pamoja na
wenzao wa G-8 watakutana katika warsha maalum itakayozungumzia
maendeleo ya kilimo duniani na ulioandaliwa na Baraza la Chicago Kuhusu
Masuala ya Dunia (Chicago Council on Global Affaris) mjini Washington na
leo Jumamosi watakutana kwenye kimji maalum cha mapumziko ya marais wa
Marekani cha Camp David katika jimbo la jirani na Washington, D.C, la
Maryland kwa ajili ya mkutano wenyewe wa G-8.
Marais walioalikwa kutoka
Afrika pamoja na Rais Kikwete mwenyewe ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
(AU) Rais Thomas Boni Yayi wa Benin, Rais John Atta Mills wa Ghana na
Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Meles Zenawi. Mkutano huo wa 38 wa
G-8 unakutanisha wakuu wa nchi za Marekani yenyewe, Japan, Ujerumani,
Uingereza, Ufaransa, Italia, Canada na Russia.
Hizi ni nchi ambazo
zimekuwa zinakutaka kila mwaka tokea mwaka 1975 wakati Rais wa wakati
huo wa Ufaransa, Mheshimiwa Giscard d’Estaing alipowaalika viongozi wa
Marekani, Japan, Italia, Uingereza na Ujerumani kujadili na kutafuta
majawabu ya mtikisiko mkubwa wa kiuchumi uliokuwa unaikabili dunia
kutokana na ongezeko la ghafla la bei za mafuta duniani kutoka nchi za
Kiarabu.
Kila mwaka, Rais mwenyeji
anapata nafasi ya kuwaalika viongozi wa nchi nyingine zikiwamo za Afrika
kuhudhuria mkutano wa G-8. Rais Kikwete alihudhuria mkutano huo
uliofanyika Japan mwaka 2008 akiwa Mwenyekiti wa AU. Sasa siyo tena
mwenyekiti wa Umoja huo. Kwa nini basi Kiongozi huyo wa Tanzania
anaalikwa katika kikao hiki muhimu pengine kuliko vingine vyote duniani?
Kuna sababu kadhaa kwa
nini aalikwe Rais Kikwete na wakaachwa marais wengine. Ni vema pia
tujikumbushe kuwa alikuwa ni Rais Kikwete ambaye alikuwa kiongozi wa
kwanza wa Afrika kualikwa na kukutana na Rais Obama katika Ikulu ya
Marekani mwaka 2008 mara baada ya Rais Obama kushika usukani wa uongozi
wa Taifa la Marekani.
Katika kufikia uamuzi wa
nchi zipi zialikwe kwenye mikutano ya G-8 ni lazima nchi hizo pamoja na
viongozi wake wawe na viwango na sifa zinazokubalika duniani. Baadhi ya
sifa kubwa ni kwamba viongozi hao wawe wamethibitisha uongozi wao katika
maeneo ya demokrasia, haki za binadamu, utulivu wa nchi na uongozi,
usalama na viwango vya kuridhisha vya maadili ya uongozi.
Katika Tanzania hakuna
shaka kuwa utawala wa Rais Kikwete umechangia sana kupanua demokrasia na
utawala bora. Hakuna shaka kuwa upo uhuru mpana zaidi katika Tanzania
ya leo iwe ni uhuru wa kisiasa, uhuru wa kiuchumi, uhuru wa kijamii
ukiwamo wa vyombo vya habari kuliko wakati mwingine wowote katika
historia ya nchi yetu.
Na wala hakuna shaka kuwa
nchi imeendelea kuwa tulivu pamoja na upanuzi mkubwa wa uhuru na
demokrasia, na wala hakuna shaka kuwa haki za binadamu zinaendelea
kulindwa na kudumishwa kwa namna iliyo ngumu sana kulinganishwa na nchi
nyingine nyingi za Afrika.
Mkutano wa mwaka huu wa
G-8 unazungumzia Maendeleo ya Kilimo Duniani na Usalama wa Chakula. Hii
ndio mada kuu. Mada hii ni sababu nyingine kwa Rais Kikwete amealikwa
kushiriki katika mkutano huo.
Tanzania chini ya uongozi
wa Rais Kikwete imekuwa mfano wa kuingwa katika jitihada za kuendeleza
kilimo. Alipoingia madarakani tu, Rais Kikwete alibuni na kuanzisha
Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo – Agricultural Sector Development
Programme (ASDP).
Mpango huu wa miaka 14
unalenga kukabiliana na changamoto kuu ambazo zimekuwa zinazuia
maendeleo ya kilimo nchini ikiwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya maji
na umwagiliaji, kuondokana na matumizi ya jembe la mkono na kuingiza
teknolojia ya kisasa, matumizi ya mbegu bora, matumizi ya mbolea zaidi,
uendelezaji wa masoko, uendelezaji wa miundombinu ya barabara za
vijijini.
Mengi yamefanyika chini ya
mpango huu. Wakulima, kwa mfano, wamekuwa wanapata ruzuku ya mbolea na
mahitaji mengine ya kilimo. Bajeti ya ruzuku hiyo imepanda kutoka sh
bilioni saba mwaka 2005 wakati Rais anaingia madarakani na kufikia sh
bilioni 121 kwa sasa.
Ili kuunga mkono malengo
makuu ya ASDP, zimeanzishwa programu nyingine kama vile Kilimo Kwanza
ambayo inalenga kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa ASDP kwa kushirikisha
sekta binafsi katika shughuli za kilimo badala ya kilimo hicho kuachwa
mikononi mwa wakulima wadogo, wa kujikimu na wasiokuwa na vyanzo vya
mitaji ya kutosha kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Katika kutafuta majawabu
ya baadhi ya matatizo yanayokikabili kilimo katika Tanzania, Serikali
tayari imeanza mchakato wa kuanzisha Benki ya Kilimo kwa kufungua
dirisha dogo la mikopo katika Benki ya Raslimali Tanzania (TIB), na iko
kwenye maandalizi ya mwisho kuanzisha Soko la Mitaji na Mazao nchini kwa
nia ya kuinua kwa kiwango kikubwa kipato cha wakulima na wawekezaji
katika sekta ya kilimo nchini.
Ili kuthibitisha dhamira
yake ya kuunga mkono malengo ya Kilimo Kwanza na ASDP, Serikali ya Rais
Kikwete imeamua kuomba mkopo wa dola za Marekani milioni 40 kutoka
Serikali ya India ambao umetumika kuagiza matreka 1,846 ambayo
yanasambazwa kwa bei ya chini na masharti nafuu sana kwa wakulima
binafsi na vikundi vya wakulima.
Mpaka sasa kiasi cha
matreka 763 yamesambazwa na hii ni mara ya kwanza katika historia ya
Tanzania kwa matreka mengi kiasi hiki kuingizwa nchini kwa nia ya
kuboresha kilimo cha Tanzania na kuondoa jembe la mkono katika shughuli
za kilimo nchini.
Kama vile hizo program
hazitoshi, Serikali imebuni program ya SAGCOT inayolenga kuendeleza
ukanda wa kilimo Kusini mwa Tanzania, ukanda ambao unaihusisha mikoa ya
Pwani, Morogoro, Iringa, Mbeya, Ruvuma na Rukwa. Program hii
inayoshirikisha Serikali na sekta binafsi ya kitaifa na kimataifa,
inalenga kuwatoa watu kiasi cha milioni mbili katika umasikini na
kuzalisha tani kwa tani za chakula na hivyo kuleta usalama wa chakula
nchini, na hata nchi za jirani.
Ilikuwa kupitia mpango wa
SAGCOT, Tanzania ikawa nchi kiongozi katika Afrika katika mpango wa
kuendeleza kilimo katika Bara hilo wa Grow Africa Partnership
unaoshirikisha nchi saba.
Kubwa zaidi katika
jitihada za kuendeleza kilimo katika Tanzania, Serikali ya Rais Kikwete
imeendelea kushikilia msimamo wa Tanzania kuibakiza ardhi mikononi mwa
Serikali na pia kulinda ardhi ya wakulima wadogo wadogo bila kuigawa
ardhi hiyo kwa wawezekaji wakubwa kwa nia ya kuimiliki ardhi hiyo bali
kwa nia ya kuikodisha kwa muda wakati wanataka kuitumia. Sera hii
sahihi, imeendelea kuifanya Tanzania nchi tofauti miongoni mwa nchi
nyingi za Afrika na hata duniani.
Kwa maneno mengine, Rais
Kikwete amealikwa kushiriki katika mkutano huu unaojadili kilimo duniani
kwa sababu amethibitisha uongozi wa kiwango cha juu katika kuendeleza
kilimo ambacho ndicho ajira kuu ya Watanzania na chimbuko la chakula kwa
ajili ya wananchi wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment