CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinaungana na familia na
wanahabari wote nchini kuomboleza kifo cha Mhariri wa Habari za Michezo wa
gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa.
TASWA
imeshtushwa taarifa za kifo cha Rachel kilichotokea usiku wa kuamkia leo, hivyo
tunatoa pole kwa familia yake, waandishi wa habari za michezo na wafanyakazi
wenzake wote, wasanii na wanamichezo wengine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa
na mdau mkubwa wa michezo na burudani.
Kutokana
na msiba huo, chama kinaandaa taratibu zake za kuwasilisha rambirambi kwa namna
tulivyojiwekea, kwani marehemu hadi mauti yanamkuta alikuwa mwanachama mtiifu
wa TASWA. Hivyo upo utaratibu kama mwenzetu akitangulia mbele ya haki namna
gani tunatakiwa tufanye.
Lakini
pia upo utaratibu mwingine nje ya chama ambao utahusu mtu binafsi kuwasilisha
michango ya rambirambi, ambapo TASWA inawasiliana na wahariri wote wa habari za
michezo wasaidie kukusanya michango ya rambirambi kwenye vyombo vyao, ambayo
wataiwasilisha kwa wajumbe wa Kamati Maalum ya kusimamia jambo hili.
Wajumbe
hao ni Angela Msangi ambaye atakuwa
Mratibu akisaidiwa na Mwani Nyangasa, ambao watashirikiana na wajumbe wa Kamati
ya Utendaji ya TASWA, George John ambaye ni Katibu Msaidizi wa TASWA, Grace
Hoka na Alfred Lucas ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji. Tunaomba
ushirikiano wa wadau katika kufanikisha jambo hili.
Msiba kwa sasa kwa mujibu wa taarifa za awali upo Manzese Tiptop,tutaendelea kujulishana kadri zitakavyopatikana taarifa mpya.
Tunaomba
waandishi wa habari za michezo, wasanii na wanamichezo kwa ujumla tumuenzi
Rachel kwa masuala mbalimbali aliyokuwa akiyatilia mkazo ikiwemo kusimamia
ukweli kwa kile alichokiamini na ndio maana tunasema tutaendelea kumkumbuka
daima. Mungu amuweke mahali pema peponi. Amin
Amir
Mhando
Katibu
Mkuu TASWA
0 comments:
Post a Comment