Nafasi Ya Matangazo

May 29, 2012

 Bw. Martin Sospeter katikati akilalamikia shutuma zilizoelekezwa kwake na bendi ya African Stars wakati alipoongea na wanahabari asubuhi hii kwenye ukumbi wa Busness Kijitonyama, kulia ni Kaimu Meneja wa bendi hiyo King Dodoo na kushoto ni Rais wa Bendi ya Mashujaa Charles Baba.

Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa Asha Baraka katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa amenifukuza kazi kutokana kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa
 
Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha nilimchukulia kama zaidi ya dada kwani nilifanya naye kazi kwa  miaka 14 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari?
 
Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutanghazwa kuhamia Mashujaa.
 
 
Leo napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mktaba wa kazi katika bendi hii.
 
“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa nafanya kazi kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo tulikaa na kukubaliana mambo mbal;imbali.
 
Mbali na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja na kunipangia nyumba hali itakayonilazimu kuhama ile iliyokuwa chini ya Twanga.
 
Ninaamini nitafanya vema kazi yangu hii mpya kama ilivyokuwa Twanga ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi mwaandishi wa habari.
Posted by MROKI On Tuesday, May 29, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo