Nafasi Ya Matangazo

May 13, 2012

GWIJI  la Taarab nchini Tanzania kutoka kundi la TOT, Hadija Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012.

Wasanii hao waliokuwa wakitumbuiza katika Tamasha maalum la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Ushirika mjini hapa.

Licha ya hali ya hewa kuwa ya mvua na manyunyu ya hapa na pale wakati wote wa tamasha hilo lakini wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake jana walivunja rekodi ya Tamasha hilo kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo tofauti na mikoa mingine ya Dodoma na Mwanza ambako tayari Tanasha kama hilo limefanyika.

Kabla ya washindi wa Tuzo za Mziki za Kilimanjaro 2012 kupanda jukwaani walianza kupandaa chipoukuzi wa tatu wealio chuana vikali na mashabiki kumpitisha Msanii Sungura aliyeonekana kupagawisha vilivyo kwa wimbo wake wa Ndizi yangu.

Walianza jukwaani kupanda washindi wa Tuzo Bora ya Wimbo wa Ragge ambayo ilitwaliwa na kundi la Warriors from East waiotamba na vibao vyao kadhaa na kupiga jukwaani zaidi ya saa moja na kibao cha Arusha Gold kilichopawa tuzo kikiburudisha vilivyo na live show yao.

Mkongwe wa Taarab, Hadija Omary Kopa aliiudhihirishia umma wa wana Kilimanjaro kuwa yeye ni Mtumbuizaji bora wa Kike baada ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo zake kadhaa zilizojaa vijembe na mashairi ya ukweli ya taarab kutoka kundi lake la TOT huku uchezaji wake ukishangilia mwanzo hadi mwisho kwa jinsi alivyokuwa akiutikisa mwili wake.

Mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT nae alipanda jukwaani nyuma ya Hadija Kopa na kutoa burudani ya nguvu na  wimbo wa  Vifuu Utundu amabao ulimpa tuzo aliucheza vilivyo na wanenguaji wake waili wa kike.

Akitanguliwa jukwaani na wacheza show wake machachari alikuwa ni mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Suma Lee aliyenyakua tuzo za wimbo bora wa Afro Pop kupiria kibao chake cha Hakunaga na Wimbo bora wa mwaka ambao pia ni hakunaga alikamua sawasawa.
 
Jukwaa lilishikwa na Omy Dimpoz kwa kuimba nyimbo zake kadhaa ikiwapo ile iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa Kushirikishwa ya Nai Nai ambapo stejini pia alipanda Ali Kiba na kumsindikiza live katika kibao hicho na kufumua yowe na shangwe kutoka kwa mashabiki.

Ali Kiba alibaki jukwaani hapo na vijana wake kumfuata kutoa shukrani zao za kupata kura zilizo wapa ushindi wa tuzo ya Wimbo bora wa Zouk Rhumba kupitia wimbo wa Dushelele. Kiba alilimudu jukwaa vyema kwa kucheza sambamba na vijana wake mwanzo mwisho.

Jukwaa lilichuliwa kwa muda na Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba na kuwashukuru ndugu zake wa Moshi kwa kumpa kura na kuwa Mchaga anaeimba vyema.

Pazia la Wasanii washindi wa tuzo za Kili Music Award 2012 wanaofabnya ziara na waliobahatika kufika mjini Mosho mkoani Kilimanjaro lilifungwa na Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani aliyeshambulia jukwaa kwa nyimbo zake kadhaa za mistaari ya maandiko.

Roma ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka.

Wasanii hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo jijini Mbeya katika uwanja wa Michezo wa Sokoine na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao wa Mkoani Dodoma na Jijini Mwanza.
Posted by MROKI On Sunday, May 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo