Hadija
Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma Mkatoliki
AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa
burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa Tuzo mbalimbali za
Kili Music 2012. Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio hilo.
Pichani juuni Mkali
wa Bongo Fleva, Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya
Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani
Kilimanjaro jana.
Barnaba
Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo
wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika
Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Roma
Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa
show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Kilimanjaro.
DJ Choka akisugua vyombo kuendanda na Roma Mkatoliki
Hapa ni usiku ....
...ni mchana
anastua...huyu ni Gwiji Hadija Kopa akifanya vitu vyake jukwaani hapo Ushirika. Mama alifunika mbaya katika show hii
Wakali
wa ragge kutoka kundi la Warriors from East la mjini Arusha wakitumbuiza
mashabiki katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye
uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro
jana.
Msanii
AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa show
maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani
Kilimanjaro jana.
Hawa nao walikuwa wakitoa mpya ya kujirusha na kuangukia mgongo. Ni vijana wa Suma Lee.
Suma Lee akifanya vitu vyake jukwaani
Msanii
anae kuja juu Omy Dimpoz nae akikamua jukwaani wakati wa show maalum ya
Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba leo.
Nai Nai hapa ikiimbwa maana Omy Dimpoz alimshirikisha Ali Kiba
Wadau wakifuatilia show hiyo
Ali Kiba akienda sawa na vijana wake, hakika Moshi ilikuwa hapatoshi
0 comments:
Post a Comment