Time Keepers wakihakikisha washindi wanapatikana kihalali.
Na.Mwandishi wetu
Kampuni na taasisi mbalimbali nchini Tanzania zimepewa wito
wa kusaidia udhami wa kusaidia mashindano yajayo ya kuogelea ili washiri waweze
kuwakilisha vyema na kuitangaza Tanzania.
Akizungumza na Mwandishi wetu Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama
hicho Bw. Marcelino Ngalioma ambaye ameandaa mashindano kuogelea kwa vilabu vyo
te vya Tanzania, amesema mashindano hayo mwaka huu yamefanikiwa sana ambapo
vilabu 250 vimeshiriki.
Amesema mwaka huu mashindano hayo yameonyesha mafikio
makubwa kwa kuwa mara ya mwisho kulikuwa na washiriki 170 pekee, lakini sasa
wamepata washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Mwanga, Moshi, Morogoro, Zanzibar
na dare s Salaam.
Aidha Bw. Ngalinoma ametoa shukrani za dhati kwa kampuni
inayojishughulisha na usambazaji wa magari ya NISSAN ya CFAO Motors kwa kutoa
udhamini ikiwa ni pamoja na kuhahakisha mchezo huo unakuwa hapa nchini.
Pia amesema hivi karibu chama hicho kitarajia kuwa na kambi
maalum kwa ajili ya wachezaji wake (Residential Camp) kwa muda wa mwezi mzima
wakijiandaa kwa mashindano yatakayofanyika Nairobi nchini Kenya.
Amefafanua kuwa Mashishindano hayo ni kwa Arika nzima na
yatakayoshirikisha vijana na pia kutakuwa na mashindayo ya wazi (Open
Chmpionship) yatakayofanyika kuanzia mwezi Septemba tehe Mosi na terehe 2.
Vilevile amesema wakati huo huo watakuwa wanamuandaa
mwogeleaji mmoja anaitwa Magdalena Moshi anayekwenda kushiriki michuano ya
Olimpiki ikiwa ni pamoja na kufanya mafunzo mikoani ili kuhakikisha mchezo huo
unaendelea nchi nzima.
Katika kuunga mkono maendeleo ya mchezo huo kampuni ya CFAO
Motors imeamua kutoa mchango wake kwa kudhamini mashindano hayo kwa kuwa imeona
ni mchezo wenye manufaa kimichezo na kiafya na huenda ukafanikiwa kulitangaza
taifa tofauti na michezo mingine ambapo kampuni kadhaa zinawekeza lakini
matunda hayaonekani.
Akizungumza Mkurugenzi wa Masoko wa CFAO Motors Bw. Alfred
Minja amesema kampuni hiyo inakusudia kufanya mazungumzo na chama hicho na
kuangalia njia watakazo tumia kuwalea na kuwaendeleza wachezaji wa mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment