Nafasi Ya Matangazo

May 10, 2012

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limepata ndege nyingine aina ya Boeing 737-500 ambayo inatarajia kuwasili leo hii (Alhamisi) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo jana ilieleza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 108 imekodiwa kutoka katika kampuni ya Aero Vista iliyopo nchini Dubai na tayari imeshafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalam kutoka katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) nchini Misri ilikoperekwa kwa ajili ya uchunguzi huo.

“Wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCCA) wamekamilisha uchunguzi wa ndege ambayo kwa sasa ipo jijini Cairo, Misri na ndege itarejea nchini kwetu leo hii mchana.

“Ndege hiyo imeshawekwa chata ya Kampuni ya ATCL na baada ya kuwasili tunetegemea itaanza kufanya safari mara moja,” Taarifa hiyo ilisema.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 12 kwenye daraja la kwanza (business class) pamoja na abiria 96 kwenye daraja la kawaida (economy class).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Bw. Paul Chizi akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wiki chache zilizopita alitoa maelezo kwa uchache juu ya ujio wa ndege hiyo lakini hakuweza kufafanua zaidi kuhusiana na ndege hiyo.

Chizi alisema kuwa mipango ya ujio wa ndege hiyo ilikuwa ni mipango ya muda mfupi iliyowekwa ili kuboresha huduma za ndege alisisitiza kuwa kampuni tayari ina mpango wa muda mrefu ambao utafanyiwa kazi kikamilifu.

ATCL hivikaribuni imezindua tovuti ikiwa katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja pamoja na kuongeza ubora wa ndege hiyo ya kitaifa.

Tovuti hiyo itawawezesha wateja kupata taarifa ya safari za ndege bila ya kufika katika ofisi za kampuni hiyo au mawakala na kuwawezesha wateja kutoa maoni yao kupitia mitandao ya kijamii.
Posted by MROKI On Thursday, May 10, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo