Kiyoyozi aina ya MULTI-V 3.
Mkrugenzi
wa kampuni ya LG kwa upande wa Tanzania akiongea na wageni waalikwa
waliofika katika uzinduzi wa Kinyoyozi kipya aina ya MULTI-V 3,
vinavyosambazwa na kampuni ya Alshaaf ambao ndiyo wakala pekee rasmi wa
kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG hapa Tanzania. Uzinduzi
huo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Fundi
mkuu wa Kampuni ya Alshaaf ambao ndiyo wasambazaji wa kiyoyozi kipya
aina ya MULTI-V 3 Bw. Emmanuel Myollah akiwahakikishia ubora wa viyoyozi
hivyo wageni waliofika katika uzinduzi huo.
Msajili Msaidizi wa bodi ya wahandisi nchini engineer Fares Washa akitoa machache katika uzinduzi guo.
Msajili
wa bodi ya wahandisi nchini engineer Steven Mlote akitoa machache
katika uzinduzi huo. Ambapo aliwashukuru kampuni ya LG kwa kuleta
teknolojia mpya ya viyoyozi aina ya MULTI-V 3 na vyenye ubora wa
uhakika.
Warembo wakifungua kwa taratibu pazia zilizokuwa zimefunika kiyoyozi huo ili kuashiria uzinduzi.
Wakiendelea kuvuta kwa taratibu.
Wakurugenzi wa kampuni ya LG na Wahandishi wa bodi ya Wahandisi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi.
Wageni wakibadilishana mawazo katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya LG wakifuatilia uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
Umati wa watu uliokuwa umefurika kufuatilia uzinduzi huo.
***
Tanzania
imechaguliwa kuwa moja kati ya nchi pekee chache barani Afrika ambapo
LG imeamua kuzindua viyoyozi aina ya MULTI-V 3, ambazo ni toleo la tatu
(tabaka la tatu) la aina ya viyoyozi aina ya VRF Air Conditioning bora
kwa matumizi ya majengo ya biashara na makazi ya saizi ya kati.
Viyoyozi
vya Multi- V 3 vinafaida tatu kwa kuu kwa watumiaji ikiwemo ufanisiwa
hali ya juu, uwezo mkubwa zaidi na faida ya kuwa na bomba refu.
Kampuni
la LG linalenga kubuni na kukuza bidhaa zinazotumia nishati kwa
ufanisi, natamka kwa kujivuna kwamba bidhaa hii itakidhi matakwa bora ya
wateja pamoja usalama wa bidhaa kutokana na teknolojia ya udhibiti
umeme na zaidi kutokana na faida za utunzaji wa mazingira kwa viwango
vya kisasa.
Alshaaf
ndio wakala pekee rasmi wa kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya
LG hapa Tanzania, naamini kwamba nchi yetu itaongoza katika kulinda
viwango vya kimataifa vya utunzaji wa tabaka la hewa na utunzaji
mazingira.
Katika
kipindi hiki cha mtikisiko wa upatikanaji nishati duniani, bidhaa za LG
zimeundwa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa zinazolinda matumizi ya
ziada ya nishati.
Tunawapongeza
washirika, LG na Alshaaf kwa jitihada zao endelevu za kutoa huduma za
ueledi za viyoyozi Tanzania kwa miaka 25 sasa na kujenga njia
inayoruhusu LG kuwa imara Tanzania kama wakala wao rasmi.
Alshaaf
ni wakala pekee rasmi wa kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG
hapa Tanzania.
Picha na Kajunason Blog.
0 comments:
Post a Comment