Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akisoma hotuba kwa niaba ya Mshauri Mwandamizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya KImbari nchini Rwanda, ambapo amehimiza nchi washiriki kuwa na imani na mahakama ya ICTR.
Wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakisikiliza Lecture ya Profesa Chris Peter Maina wakati wa mjadala wawazi wa kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Mwaka 1994.
Balozi Mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Sano Lambert akitoa neno la shukrani na pia kuasa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutetea amani na maendeleo kwa faida ya vizazi vijavyo na maendeleo ya ukanda wa Maziwa makuu kwa ujumla.
Profesa Chris Peter Maina wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akielezea na kufafanua umuhimu wa Mahakama, akitolea mfano ya ICTR kushirikiana na Taasisi na Mashirika ya Kijamii katika kuhakikisha haki inatendeka, haswa katika matukio kama ya uhalifu wa kivita.
Wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichangia mada katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini tujifunze kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
Katibu Daraja la Kwanza wa Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania Bw. Ernest Bugingo akisisitiza jambo na kuwataka wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujifunza zaidi na kusoma makala za mauaji ya Kimbari kupitia mtandao.
Wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichangia mada katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini tujifunze kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
nasemaje? it never happen again. haitatokea tena au,kamwe.mdau kigali makazi yake boksini
ReplyDelete