KAMATI ya Miss Tanzania kupitia kampuni ya Lino International Aggency ikishirikiana na Redds, leo inafanya semina kwa waandaaji wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012 kwa ngazi za Kanda na Mikoa. Semina hiyo ya siku mbili inafanyika katika Ukumbi wa Kifaru uliyopo Hoteli ya Giraffe Ocean View nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Pichani ni baadhi ya waandaji hao wakiwa tayari ukumbini kusubiri kuanza kwa semina hiyo, Mwandaaji wa Arusha Ruth Ibrahim, Mwandaaji wa Katavi na Rukwa, Mariam Amir, Mwandaaji wa Dodoma, Doris Kayombo, Mwandaaji wa Elimu ya Juu Dodoma, Evans Exaud, na Mwandaaji wa Mtwara Rajab Mchatta.
Hapa ni mwandaaji wa Lindi Shaha Ramadhan akiwa na Mwandaaji wa Elimu ya Juu Morogoro, Verdiana Kamugisha ambaye pia alikuwa Miss Tanzania 2 mwaka 2004.
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na maofisa wa Kamati ya Miss Tanzania, Aidan Rico (katikati) na Yasson Mashaka.
Mwandaaji wa Njombe, Slyvia Mwakilufi, Mwandaaji wa Kanda ya Mashariki, Alex Nictas na Mwandaaji wa Mtwara Rajab Mchatta.
Mwandaaji wa Mkoa wa Ruvuma, Issa Shamte (kulia) akiwa na Mwandaaji wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Erick Mfugale.
Mwandaaji wa Mkoa wa Geita, Redrose Gabriel akiwa pamoja na Mwaandaaji wa Simiyu, Innocent Mafuru (katikati) na Mwandaaji wa Kurasini Sam Mshana.
Mwandaaji wa Miss Elimu ya Juu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Lemina Mkawa akiwa na Mwandaaji wa Mbeya, Amani Mbilo.
Miss Tanzania 2011, Salha Izrael (kushoto) akiwa na Mwandaaji wa Miss Kinondoni, Husna Maulid ambaye pia alikuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2011.
0 comments:
Post a Comment