Nafasi Ya Matangazo

March 29, 2012

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao pia ni Waandaaji wa Redds Miss Tanzania 2012, Hashim Lundenga akifungua rasmi semina ya mawakala wa Miss Tanzania 2012 jijini Dar es Salaam hii Leo. Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, kutoka Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) Victoria Kimaro.
Lundenga alisema kuwa Kamati hiyo kupitia wadhamini wamedhamiria mwaka huu kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya Urembo nchini na waandaaji pia wamedhamiria kupata warembo bora watakao shiriki shindano hilo la urembo mwaka huu.
Lundenga pia alitoa kaulimbiu ya mashindano hayo kwa mwaka huu kuwa ni “MSHINDI BORA, MWAKILI BORA MWENYE SIFA BORA”
Mawakala wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012 wakiwa katika chumba cha mkutano wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Hashim Lundenga Mkurugenzi wa Miss Tanzania.
Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Oscar Makoye (kushoto) akisoma utaratibu utakao tumika katika semina hiyo ya mawakala . Kulia ni Ofisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania na MC wa shughuli hiyo, Aidan Rico.
Posted by MROKI On Thursday, March 29, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo