Mkuu wa Mkoa wa Iringa , Dk. Christine Ishengoma akikata utepe leo kuzindua maadhimisho ya wiki ya maji yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti nka Kitaifa Mkoani Iringa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya wiki ya Maji ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji-Idara ya Maji jijini, Amani Mafuru pamoja na maofiwa Mkoa wa Iringa.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda(kushoto) akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ambao ndio wadhamini wa wiki ya Maji kitaifa lililopo katika uwanja wa Samora yanapoendelea maonesho hayo. Katikati ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa SBL, Nandi Mwiyombela.
Mahusiano ya Jamii wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Nandi Mwiyombela akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ambao ndio wadhamini wa wiki ya Maji kitaifa lililopo katika uwanja wa Samora yanapoendelea maonesho hayo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dk Christina Ishengoma akipata maelezo kutoka kwa Hamdar Chanzi Mkemia mwandamizi Maabara ya maji Iringa, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maji vijijini Wizara ya maji na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi maadhimisho ya wiki ya maji Amani Mafuru
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma wakati akipita katika mabanda ya maonesho na kupata maelezo kuhusiana na shughuli za taasisi hizo.
Chuo Kikuu cha Tumaini cha Mjini Iringa nacho kipo kinashiriki maonesho hayo. Pichani ni wanafunzi wa chuo hicho wakisubiri mgeni rasmi apite.
Mgeni rasmi alipita katika mabanda ambayo yanavifaa vya kuhifadhia maji na mengine ambayo yanahusika na usafishaji maji ili yaweze kutumika katika matumizi ya binadamu.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma akihutubia wananchi wa mjini Iringa waliohudhuria ufunguzi huo wa maonesho hayo ya wiki ya maji kitaifa.
RC akiangalia maonesho ya sarakasi
Wananchi waliohudhuria ufunguzi huo wa wiki ya maji kitaifa wakimsikiliza Mgeni rasmi. Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo ni “Maji kwa Usalama wa Chakula” huku wadhamini wakiwa ni Kampuni ya Bia ya Serengeti.















0 comments:
Post a Comment