Nafasi Ya Matangazo

March 19, 2012

 Mhandisi wa Maji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoani Iringa , Anna Bugoro akiwaeleza jambo wanwa Shule za MsinMlandege na Jitegemee mkoringa wanaosoma darasa la pili juu ya usafishaji maji unavyo fanyika wakati wa maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya maji Kitaifa yanayoendelea Mkoani Iringa.
Mmoja wa wakazi wa Mjini Iringa akipatiwa maelezo juu ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Maji alipotembelea banda la SBL leo katika viwanja vya Samora mjini Iringa.
 Watoto wa shule ambao ndio kizazi kinachopaswa kupewa elimu bora ya matumizi ya maji sahihi na namna ya kuhifadhi maji na vyanzo vya maji, wakimsikiliza mtaalam kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji juu ya madini yanayopatikana katika maji na kuleta madhara mbalimbali kama kuoza meno, ulemavu na kichwa kikubwa.
 Watoto wa shule wakifurahia kupigwa picha baada ya kukusanya Vipepereshi mbalimbali vya masuala ya maji, walipotembelea maonesho ya Wiki ya Maji mjini Iringa leo
Mtaalam wa maji kutoka Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Florentina Didas (aliyekaa kushoto-juu na aliyesimama kushoto picha ya chini) akiwaelekeza wakazi wa Iringa waliotembelea banda hilo juu ya mchezo wa uhifadhi mazingira na vyanzo vya maji unavyochezwa.

Wananchi wakiwa katika banda la TAWASANET wakijipatia maelezo mbalimbali juu ya shughuli zao.
Posted by MROKI On Monday, March 19, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo