Nafasi Ya Matangazo

February 28, 2012

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kulia), akifunua pazia  kuonesha jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa mtambo wa nne wa  usafishaji maji yaliyotumika kiwandani kuwa maji salama kwa matumizi   ya binadamu katika hafla iliyofanyika katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia  Tanzania (TBL) cha Arusha, mwishoni mwa wiki.Anayeshuhudia uzinduzi  wa mtambo huo uliogharimu sh. bilioni  3.6, ni Mkurugenzi Mtendaji wa  TBL, Robin Goetzsche.
Msimamizi wa Mtambo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa kusafisha maji  taka kuwa salama kwa matumizi ya binadamu, Said Lwambo kutoka   Kampuni ya Talbot & Talbot, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa   Arusha, Magesa Mulongo (wa pili kushoto) na Waziri wa Viwanda na   Biashara, Cyril Chami (wa tatu kushoto) kuhusu usalama wa maji hayo  wakati wa uzinduzi wa mtambo huo uliogharimu sh. bil 3.6 ambao  ulifanyika hivi karibuni katika kiwanda cha TBL Arusha.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kulia), akisalimiana na  viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), alipowasili katika hafla ya uzinduzi wa mtambo wa nne wa usafishaji maji yaliyotumika kiwandani  kuwa maji salama kwa matumizi ya binadamu katika Kiwanda cha  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, mwishoni mwa wiki.Kutoka  kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL, Gavin van Wijk, Meneja wa   Kiwanda TBL Arusha,Bert Grobbelaar na  Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,  Robin Goetzsche. Wa pili kulia ni Waziri wa viwanda na Biashara ,Dk.  Cyril Chami.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, akihutubia wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto), akifurahia jambo walipokuwa wakitembelea mtambo huo.
Posted by MROKI On Tuesday, February 28, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo