
Waratibu wa Ukimwi katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Lindi na Mtwara wapo kwa ajili ya kuwaelezea masuala mbalimbali washiriki wa semina hiyo, kuhusu maambukizi ya ukimwi na kupambana na janga zima la Ukimwi linalotishia jamii na nyanja mbalimbali za kiuchumi nchini Tanzania kutokana na kudhoofisha nguvu kazi ya Rasirilimali watu.
Semina hiyo imeandaliwa na Taasisi ya kuzuia ukimwi TACAIDS ikishirikiana na kampuni ya Masoko Agency ya jijini Dar es salaam na tayari imeshafanyika katika kanda Kaskazini Arusha, Kanda ya Ziwa Mwanza, Kanda ya Kati Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya na sasa ni Kanda ya Mashariki Mjini Kibaha






0 comments:
Post a Comment