Nafasi Ya Matangazo

February 28, 2012

Mazishi ya Marehemu Jasper Bitwale (pichani),aliyekuwa Ofisa Elimu wa Manispaa ya Morogoro mjini upande wa sekomndari yamefanyika leo kijijini kwake Murgwanza Wilayani Ngara mkoani Kagera.

Marehemu Bitwale alifariki Jumamosi Februari 25,2012 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa Jumatatu kutoka mkoani Morogoro baada ya kuagwa na maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji vyake, ambako kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi kama Mwalimu wa Sekondari Mzumbe, kabla ya kuhamishiwa Gairo na baade Tabora na kurejea kuwa Afisa Elimu Manispaa ya Morogoro.Marehemu Bitwale ambaye pia ni Kada wa Chama cha Mapinduzi na aliwahi kuonesha nia yake ya Kugombea Ubunge jimbo la Ngara katika kura za maoni za CCM jimbo la Ngara lakini kura zake hazikutosha. 

Waliokuwa wakigombea pamoja na Marehemu wakati huo ni pamoja na Prof Fedhman Banyikwa, Joseph Rugumyamheto, Deo Ntukamazina, Elam Ruzika, Jaspa Bitwale, Dr. Bujali, Alex Gashagha, Gwasa Sebabiri, Muhuranyi na Anna Nyamubi. 

 Marehemmu ameacha Mjane na watoto wa tatu. 
Blogu hii inaungana na wote waliofikwa na msiba huu kuwapa pole. 
Posted by MROKI On Tuesday, February 28, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo