TAARIFA KWA UMMA:Usiku wa leo majira ya saa 8 nikiwa natoka kwenye mizunguko yangu nikielekea home Mbezi kwa Msuguri, nilipofika maeneo ya Kimara resort nikakuta mtu ameanguka barabarani huku pikipiki ikiwa juu yake, nikasimama ghafla kwa umbali wa kama mt 10 nikiwa na tathmini kama ni kweli ninaona ajali. Nilipokuwa napepesa macho kwa pembeni ya barabara nikamuona mtu mwingine kalala chali nikajiridhisha kwamba watakuwa wameanguka na yule kutupwa. Nikashuka kwa tahadhari niliposogea km hatua 5 nikakumbuka nyuma kidogo nilipita pikipiki ilipokuwa imeegeshwa pembeni bila ya mtu juu wala embeni nikashtuka na nilipo geuka kwa mbali kizani nikaiona inakuja kimya kimya bila kuwashwa na bila mwanga nikagundua utakuwa mtego kwa speed ya rhocket nika rudi kukimbilia gari yangu na ndipo mwenye pikipiki naye akawasha kuja kuniwahi, ikanibidi ni mtishie kama nina mrukia akanikwepa na mimi nikarukia kwenye gari yangu. Kwa kuwa ilikuwa silence nika tia gear nikiwa tayari kuwagonga kama wangejaribu kunibugudhi mara wale wengine nao wakadandia yao nakuanza kukimbia nikajaribu kuwafukuza niwagonge japo kidogo wakaingia barabara ya vichochoroni nikajirudia zangu.
Jamani hii ndo Tz yetu sasa, msaidie tu yule unayemfahamu... Siku njema!By Macmillan George
TAARIFA KWA UMMA:
Usiku wa leo majira ya saa 8 nikiwa natoka kwenye mizunguko yangu nikielekea home Mbezi kwa Msuguri, nilipofika maeneo ya Kimara resort nikakuta mtu ameanguka barabarani huku pikipiki ikiwa juu yake, nikasimama ghafla kwa umbali wa kama mt 10 nikiwa na tathmini kama ni kweli ninaona ajali. Jamani hii ndo Tz yetu sasa, msaidie tu yule unayemfahamu... Siku njema!
By Macmillan George
0 comments:
Post a Comment