Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature pichani kati akishiriki uzinduzi wa Airtel Money ndani ya mji wa Dodoma jioni ya leo kwenye uwanja wa Jamhuri,ambapo watu mbalimbali walijitokeza kwa wingi kulishuhudia tukio hilo adhimu,kulia ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando na kushoto ni Meneja wa Airtel Money-Tanzania,Asupya Bussi Nalingingwa.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la Wanaume Halisi kutoka TMK,likiongozwa na Juma Nature wakilishambulia jukwaa vilivyo,kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya Airtel Money,uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wati kibao.
Mmoja wa sanii mahiri wa miondoko ya hip hop hapa bongo,Hamis Mwinyjuma a.k.a Mwana FA akiwapagawisha baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika jioni ya leo kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya Airtel Money,uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wati kibao.
Anajiita Simba Dume ndani ya msitu mnene,ni mmoja ya Wasanii wakongwe wa hip hop hapa nchini,ndani ya miondoko ya muziki wa kizazi kipya,Mfalme wa rhymes Afande Sele pichani kati akiwa amezungukwa na washabiki wake,huku akiwaimbia wimbo wake wa Karata Dume, shangwe na miluzi ikiwa imetawala uwanjani hapo jioni ya leo,wakati kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Money kwa wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya leo.
Wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi jioni ya leo kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money kutoka kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel wakishangilia
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Q-Chilla a.k.a Savimbi akiwaimbisha washabiki wake jioni ya leo kwenye uwanja wa Jamhuri wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money.
Mmoja wa wasanii wa miondoko laini laini hivi,aitwaye Mr Blue a.k.a Kabaisa akitumbuiza jukwaani jioni ya leo kwa wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la uzinduzi wa Airtel Money.
Namna shangwe za Aitel Money zilivyokuwa zikilindima usiku huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Pichani juu ni baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi jioni ya leo kwenye uwanja wa Jamhurimwakati kampuni ya simu ya Airtel,ilipokuwa ikizindua huduma yake ya Airtel Money,ambapo wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi kwenye tukio hilo na kuipokea kwa shangwe huduma hiyo.
0 comments:
Post a Comment