Nafasi Ya Matangazo

December 09, 2011

 Mwanafunzi wa Kidato cha Tano Janeth Absalom kutoka Loyola High School akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
 Afisa Habari wa UN Information Centre (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwakaribisha wageni waalikwa katika semina ya mafunzo kwa vijana juu ya matumizi ya mtandao katika kuhamasisha haki za Binadamu iliyofanyika  katika Ofisi za UN Information Centre.
 Mtaalamu wa IT na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu kutoka  Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Bw.Wilfred Warioba akielezea jinsi mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano kama vile Facebook, Twitter na Blogs zinavyofanyakazi na zinavyoweza kutumika kupashana Habari na Kuelimishana ambapo pia amesema iwapo itatumika vibaya inaweza kuelta madhara makubwa kwa watumiaji. Katikati ni Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG  Bw. Ayoub Rioba na Afisa  Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo.
 Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG  Bw. Ayoub Rioba akielezea nafasi ya vijana kama wahusika wakuu katika matumizi ya Mitandao hiyo ambapo amewataka vijana kuwa watetezi wa haki za Binadamu kwa kutoa taarifa pale wanapoona haki hizo zinakiukwa.
 Wanafunzi na wageni waalikwa waliohudhuria mafunzo hayo wakitazama filamu "White and Blacks: Crimes of Color" inayozungumzia Maisha, Haki na Adha wanazokabiliana nazo jamii ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino).
 Afisa Habari wa Temeke Youth Development Network (TEYODEN) Humphrey Shao akifafanua jambo kuhusiana na matumiz ya mitandao kama njia ya mawasiliano
 Wanafunzi na wageni waalikwa waliohudhuria mafunzo hayo wakitazama filamu "White and Blacks: Crimes of Color" inayozungumzia Maisha, Haki na Adha wanazokabiliana nazo jamii ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino).
Afisa Habari wa United Nationa Information Centre Usia Nkhoma akigawa nakala za Filamu ya "White and Black: Crimes of Color". kwa wanafunzi wawakilishi wa shule zilizohudhuria mafunzo hayo.
Posted by MROKI On Friday, December 09, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo