Nafasi Ya Matangazo

December 13, 2011

                  Mchungaji Kiongozi wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima (Glory of Christ Ministries      International) Mch. Josephat Gwajima, atakuwepo Jijini London Jumatano-Tarehe 14 Disemba 2011 kwa ajili ya Mkutano wa Injili. Mkutano utaanza saa 12 jioni baada ya saa za kazi.

            Watanzania wote waishio Jijini London, mnaombwa kuhudhuria Mkutano huu wa Injili ambapo Mchungaji Josephat Gwajima, atakuwepo kuhubiri neno la Uzima, kuombea wagonjwa, kufungua wote walioneewa na ibilisi na kuwaweka huru wale wote waliofungwa katika magereza ya Kiroho.

Uonapo Tangazo hili mfahamishe na mwenzio! Kama una ndugu, jamaa na marafiki waishio London nao pia unaweza kuwataarifu ili wapate fursa ya kukutana na Mtumishi wa Mungu, Mch. Josephat Gwajima.

Ili kuhudhuria Mkutano Huu Fuata Anuani hii:-

GLORY OF CHRIST MINISTRIES INTERNATIONAL
LANGHAM ROAD
TOTTENHAM, LONDON
N15 3RB
+44742753204

Imetolewa na :

Huduma ya Taarifa (Information Ministry) ya Glory of Christ Ministries International
Posted by MROKI On Tuesday, December 13, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo