Nafasi Ya Matangazo

December 19, 2011

Habari kutoka Dodoma katika mkutano wa CUF zinapasha kuwa moto wazidi fuka katika vyama vya upinzani nchini ambapo katika mkutano wa CUF mjini Dodoma wanachama wanazidi Muunga mkono Mbunge wa Wawi Hamad Rashid na kutaka Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kujivua gamba.

Wanachama wa CUF Wilaya ya Dodoma wanadai hivi sasa chama hicho kimefunga ofisi zake karibu mikoa yote kwa kukosa fedha za pango jambo ambalo linatokana matumizi mabaya ya fedha. 

Wakitolea mfano matumizi ya fedha za uchaguzi katika Jimbo la Igunga, wamedai matumizi hayakuwa mazuri hivyo wanataka  fedha iliyobaki katika Kampeni ya Uchaguzi jimbo la Igunga ijulikane imekwenda wapi maana CUF ilitenga Tsh Milioni 800 kwaajili ya Uchaguzi huo lakini zilizotumika ni Milioni 300 pekee hivyo wanataka kujua wapi zilipo Milioni 500.

Aidha wanachama hao wanadi kutoka kuwajibika ipasavyo kwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ndio chanzo kwa kuzorota kwa CUF mikoani, hasa kutojkana na kuto kufanya kwa ziara za mara kwa mara. Walidai hivi karibuni baada ya kulalamika ndio katembelea mikoa ya Lindi na Mtwara.

Posted by MROKI On Monday, December 19, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo