Daladala licha ya kuandikwa ruti ya G/MBOTO Kariakoo lakini hufanya kazi ya kubeba abiria kati ya Ukonga Mombasa hadi Moshi Bar na KwaMkolemba jijini Dar es Salaam kupitia njia ya Mazizini. Pichani ni daladalahilo likipita katika mabwawa ya maji yaliyopo katika barabara hiyo ambayo imechimbika na kuwa kero kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo kiasi cha wakazi wengi kujiuliza je barabara hiyo ipo jijini Dar es Salaam au vijijini.
Hii ndio hali halisi ya barabara hiyo ambayo kutokana na ubovu wake hivi sasa abiria hulazimika kulipa nauri ya Sh 500 badala ya ile ya 300 ya awali. na magari mengi ambay9o ni mabovu yameshindwa kabisa kufanya kazi.
Magari madogokama haya yaliyo na hitilafu yanashindwa kupita na kuamua kugeuza na kurudi yalipotoka. Rais Kikwete wakati wa Kampeni zake alifika Moshi Bar na kuwaahidi wakazi wa maeneo hayo kuwapindi wakimchagua ujenzi utaanza mara mojalakini hadi sasa ni ndoto.Mbunge wa Ukonga, Egune Mwaiposa nae yupo
Mvua pia zina haribu miundombinu
0 comments:
Post a Comment