Mkali wa muziki wa hip hop kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini,Mfalme wa Rhymes ,Simba Mzee,Afande Sele akiwarusha vilivyo wakazi mbalimbali wa jiji la Mbeya,waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel,Airtel Money uliofanyika leo kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Sokoine.
Wakazi wa jiji la Mbeya kutoka vitongoji mbalimbali wakishangilia vilivyo jioni ya leo kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya Airtel Money,lililofanyika katika uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Jaffarai akitumbuiza jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma mpya kutoka kampuni ya simu ya Airtel,ijulikanayo kwa jina la Airtel Money.Ilikuwa shangwe mwanzo mwisho,wakazi wa Mbeya wameipokea vyema huduma ya Airtel Money.
Palikuwa hapatoshi leo kwenye uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya.
Kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Temeke,Wanaume Halisi likiongozwa na kinara wao Juma Nature wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani ya uwanja wa Sokoine,kwenye uzinduzi wa huduma mpya itolewayo na kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel,ijulikanayo kwa jina la Airtel Money,ambapo wakazi wa jiji la Mbeya wameipokea kwa shangwe.
Jukwaani ni wakali wa miondoko ya hip hop katika muziki wa kizazi kipya,kulia ni Jaffarai pamoja na Jay Mo wakikamua vilivyo jukwaani kwenye tamasha la Bongo 50,lililodhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel,kupitia huduma yao mpya ya Airtel Money.
0 comments:
Post a Comment