Nafasi Ya Matangazo

November 11, 2011

 Zao la nynya ndio zao kuu la biashara kwa wakazi wa Kijiji cha Kipera na vitongopji vyake. Wakazi wengi wa  kijiji hicho kilichopo Kata na Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro hulima nyanya kwa wingi msimu wa kilimo unapowadia na na wafanya biashara hufika kijijini hapo na kununua zao hilo na kusafirisha hadi jijini Dar es Salaam au mikoa mingine.
 Pichani ni moja ya kijana mkazi wa kijiji cha Kipera ambaye mbali na kulima zaio hilo anasema msimu ukifika ni ajira kwa kila mtu kijijini hapo alimaye na asiyelima nyanya. Anasimulia kuwa wapo ambao hujishughulisha na uvunaji wa nyanaya mashambani, usombaji kutoka shamba hadi vilinge vya wafanya biashara, upangaji katika matenga kama afanyao yeye na upakiaji katika magari. Pia anasema wapo wanaofanya kazi ya kukata majani kwaajili ya kupangia nyanya hizo katika matenga.

Pia anasema msimu wa mavuno ya nyanya wafanya biashara wengi hufika kijijini hapo hivyo akina mama na watu mbalimbali hufungua migahawa ya chakula na kufanya pato la wakazi wa kijiji hicho kukua kipindi hicho. 

Lakini analia na bei ambayo mkulima huopata ambapo tenga moja la kuingia plkastiki 3 za lita 20 hununuliwa klwa kati ya Tsh 5,000 na 8,000/=  hivi sasa kulingana na ubora wa nyanya uliyonayo. Ipo haja ya serikali kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa soko na kiwanda cha kusindika nyanya kijijini hapo ili kukuza kipato cha wakazi wa Kijiji cha Kipera.
Nyanya hii ikifika jijini Dar es Salaam huuzwa kwa bei ya juu sana.
Posted by MROKI On Friday, November 11, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo