Nafasi Ya Matangazo

November 24, 2011

Mvua kubwa iliyonyesha Mkoani Manyara alfajiri ya kuamkia leo imesababisha maafa baada ya wawu wa wawili kufa maji baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji katika eneo la Makuyuni Mkoani Manyara.

Lori la mizigo Scania Semi Trela lililokuwa limepakia Caterpillar na watu watano ndanbi yake lililosombwa namaji katika eneo hilo na kusababisha vifo vya watu wawili huku wawili wengine wakijeruhiwa na mmoja kunusurika baada ya kuwahi kuruka. 

Aidha gari lingine dogo aina ya Toyota Corola lilisombwa na maji hayo na dereva wake kunusurika kifo.

Mbali na hali hiyo pia maji hayo yamesababisha athari kubwa ya kipande cha barabara kukatika katika daraja la makuyuni jambo ambalo lilisababisha kufungwa kwa muda kwa njia hiyo kabla ya kufunguliwa baade kwa magari kupita upande mmoja wa barabara hiyo ya Arusha Karatu.


Picha zaidi za tukio hilo zitakujia hapo baade. 
Posted by MROKI On Thursday, November 24, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo