Nafasi Ya Matangazo

November 17, 2011

Makocha Wazawa walioteuliwa kukinoa Kikosi cha timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa akishirikiana na Kocha Msaidizi wa Kikosi hicho Jamhuri Kihwelu "Julio" wameteua wachezaji 28 kuunda kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji inatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 mwaka huu.
 
Akiwataja Mbele ya waandishi wa Habari hii leo , Kocha Msaidizi wa kikosi hicho Julio, aliwataja Wachezaji walioteuliwa kuwa ni Juma Kaseja (Simba), Deo Munishi (Mtibwa Sugar) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni Shomari Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba) na Paul Ngelema (Ruvu Shooting).
 
Mabeki wa kati ni Juma Nyoso (Simba), Said Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Salum Telela (Moro United). Viungo ni Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mwaipopo (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Haruna Moshi (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Rashid Yusuf (Coastal Union), Jimmy Shogi (JKT Ruvu Stars) na Mohamed Soud (Toto Africans).
 
Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Gaudence Mwaikimba (Moro United), John Bocco (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Daniel Reuben (Coastal Union) na Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada).
 
Kwamujibu wa Julio amesemka kisi hicho kinaingia kambini mara moja na mchujo utafanyika kwa kuengua magarasa 8 hivyo kiksi kitakachoshiriki mashindano hayo kitaundwa na wakali 20 pekee.
Posted by MROKI On Thursday, November 17, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo