Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga (kushoto) akimsikiliza Afisa Masoko wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Marecha Edward (kulia) wakati alipotembelea Moja ya minara ya mawasiliano ya Airtel uliopo Muheza,Mkoani Tanga mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya Ziara yake katika Mkoa wa Tanga.Katikati ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" akionyesha simu yake kwa Afisa Masoko wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Marecha Edward wakati kampuni hiyo ilipotembelea kijiji cha Bombo Maji Moto,Kata ya Kizari wilaya ya Korogwe Vijiini ili kuona hali ya mawasiliano ilivyo wakati wa ziara ya Maalum ya Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga mwishoni mwa wiki (hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga (wa pili kulia) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" (kushoto) wakimsikiliza mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kijango Magoma,aliejitambulisha kwa jina la Mzee Khalifa (mwenye kofia) alipokuwa akielezea hali ya mawasiliano katika kijiji hicho wakati wa ziara maalim ya Naibu Waziri ya kuangalia hali ya mawasiliano wilayani humo.Kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Marecha Edward alieambatana na Naibu Waziri kwenye ziara yake hiyomwishoni mwa wiki .
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Chiku Gallawa (kulia) akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga (wa pili kulia) ambaye aliambatana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya pamoja na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Marecha Edward walipokuwa wakitathmini hali ya Mawasiliano ya simu za mkonini na jinsi ya kuyaboresha katika mkoa huo wa Tangamwishoni mwa wiki .
0 comments:
Post a Comment