Nafasi Ya Matangazo

October 21, 2011

Ujumbe maalum kutoka nchini Marekani, Viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete baada ya kumaliza mazungumzo na ujumbe huo hii leo. Ujumbe huo ulizunpamoja na mambo miengine ni  jinsi ya kusaidia kuwaletea vifaa  vya tiba kwaajili ya kusaidia kupunguza vifo ya wakinamama na watoto wachanga nchini .

Taasisi ya General Election Health Magination (GE) ya nchini Marekani imeamua kufanya kazi na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ili kuhakikisha kuwa vifo vya wanawake wajawazito na watoto vinapungua hapa nchini.
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi hiyo Janeen Uzzell wakati akiongea na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Uzzel alisema kuwa wameamua kufanya kazi na Taasisi ya WAMA kutokana na jitihada zinazofanywa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mama Salma Kikwete  za kuhakikisha kuwa vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinapungua kwa kuchangia vifaa tiba katika Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati  na kutoa elimu ya uzazi salama kwa jamii.
“Katika suala la kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto Taasisi yetu inafanya kazi tatu ambazo ni kufuatilia maendeleo ya Mama mjamzito tangu mimba iko changa hadi wakati wa kujifungua, tunatoa  mashine ya kumsaidia mtoto mchanga na mama mjamzito pale ambapo mama atakuwa amejifungua na hana nguvu za kumsaidia mtoto na vifaa tiba vya kuwahudumia wagonjwa wa dharula”, alisema Uzzell.
Kwa upande wake Mama Kikwete aliishukuru taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa kuimarisha afya ya mama na mtoto na hivyo kuamua kufanya kazi  nchini Tanzania kwa ajili ya kukabiliana na  tatizo hilo.
Alisema kuwa Afrika inahitaji kusaidiwa ili iweze kuimarisha afya ya mama na mtoto kwani vifo vya mama na mtoto ni tatizo katika nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania  ili kukabiliana na tatizo hilo Serikali inafanya kila liwezalo ili kuhakikisha kuwa  malengo ya milinia namba  nne na tano yanafanikiwa ifikapo mwaka 2015.
 
Posted by MROKI On Friday, October 21, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo