Nafasi Ya Matangazo

October 23, 2011

Meneja wa bia ya Tusker Rita Mchaki (kulia) wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) akiteta jambo na Meneja wa Tukio la Dar es Salaam Quiznite World Vincent Aduor katika hafla ya tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam na kudhaminiwa na kinywaji cha Tusker Malt.
Meneja wa Tukio la Dar es Salaam Quiznite World Vincent Aduor (kushoto) akimkabidhi fedha taslimu sh. mil. 1/= nahodha wa kundi la Mwananchi Jullie Masiga baada ya kuibuka washindi wa kujibu maswali katika tukio la Dar es Salaam Quiznite World lililofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam na kudhaminiwa na kinywaji cha Tusker Malt.Anayeshuhudia kulia ni Meneja wa Tusker Malt Rita Mchaki na wengine ni wajumbe wa kundi hilo.
Meneja wa bia ya Tusker Rita Mchaki (katikati ) wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) akiwa katika picha ya pamoja na kundi la Chondechonde baada ya kuwakabidhi zawadi zao kwa kushika nafasi ya tatu kujibu maswali katika tukio la Dar es Salaam Quiznite World lililofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam na kudhaminiwa na kinywaji cha Tusker Malt.

 ***********************
TUKIO la burudani la Dar es Salaam Quiznite lililofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki lilifana kwa kiasi kikubwa ambapo burudani ya muziki na sarakasi ziliteka mashabiki waliofika katika tukio hilo.

Pamoja na burudani tukio hilo lilihusisha mashindano ya kujibu maswali katika nyanja za muziki, michezo,elimu ya uraia na filamu ambapo washiriki waliunda makundi ya watu kumi kumi yalioingia katika mchuano.

Katika mchuano huo kundi la Mwananchi liliibuka washindi na kujinyakulia fedha taslimu sh. mil 1/= na kundi lililojiita Synovate liliibuka kuwa washindi wa pili na kundi la Chondechonde lilishika nafasi ya tatu na kujinyakulia zawadi kutoka kwa wadhamini.

Meneja wa kinywaji cha Tusker Malt waliodhamini tukio hilo alisema kampuni yake imefarijika na muitikio wa watu katika tukio hilo ambalo ni jipya katika jamii ya kitanzania.

Alisema Dar es Salaam Quiznite imetokana na tukio la kidunia linalojulikana kama Quiznite World linalofanyika katika nchi mbalimbali likiwa na lengo la kuwakutanisha watu wa rika mbalimbali na nyanja tofauti katika kubadilishana mawazo.

“Hii ilikuwa nafasi nyingine kwa wanywaji wetu kupata wigo mpana wa kuwa karibu na kinywaji cha Tusker Malt katika burudani ambayo itawasaidia kujenga mahusiano baina yao na marafiki zao ndani ya sekta tofauti”, alisema Mchaki.

Kwa upande wake Meneja wa Quiznite World Vincent Adour alisema anaamini uwanja huo wa majadiliano ni nafasi nzuri ya kujifunza kutoka kwa wengine ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa kufahamiana na wakati fulani kupanua soko la biashara.

Alisema tukio hilo sasa litakuwa linafanyika Tanzania katika kipindi cha kila robo mwaka na kwamba wanaamini tukio litakalofuata litakuwa kubwa zaidi na kuwavutia wengi kushiriki.

"Dar es Salaam Quiznite imefungua milango kwa matukio mengine yatakayofuata kwani tunaamini matukio yatakayofuata yatakuwa na wigo mpana zaidi wa ushiriki," alisema Adour.
Posted by MROKI On Sunday, October 23, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo